22.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

SSMC yatangaza neema kwa vijana Tanga

Oscar Assenga, Tanga

Kampuni ya SSMC Limited ya jijini Tanga ambao ni wasambazaji wa bidhaa za Oil zinazotengenezwa na Mogas Tanzania Limited imepanga kutoa ajira kwa vijana mkoani humo kwa kuwapa nafazi za kazi katika kampuni hiyo.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Mei 2, Msambazaji Mkuu wa Kampuni hiyo mkoani Tanga Saidi Kijiko amesema wakiwa kama wakala mkuu wa kusambaza bidhaa za kampuni hiyo wameona watumie fursa hiyo kutoa ajira kwa vijana.

Amesema wamedhamiria kuhakikisha wanazalisha ajira za kutosha ili kuweza kuwaondoa vijana vijiweni ambao pia wamekuwa wakitumia muda huo kufikiria kufanya vitendo viovu kwenye jamii.

“Niwaambie tu kwamba tumedhamiria kuhakikisha tunapunguza tatizo la ukosefu ajira kwa vijana mkoani Tanga kwa kuwapa nafasi ya kufanya kazi kwenye kampuni yetu lengo kubwa ni kuwawezesha kupata kipato cha kuendesha maisha yao,” amesema.

Hata hivyo amesema ili kuhakikisha wanawawezesha vijana wanakusudia kufungua maduka kwenye Wilaya mbalimbali mkoani Tanga ili kuweza kutoa fursa ya ajira kwao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles