20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Tyga: Nilikuwa tayari kumfanyia lolote Kylie

Tyga na KylieNEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Tyga, amefunguka na kusema kwamba alikuwa tayari kufanya lolote kwa aliyekuwa mpenzi wake mwanamitindo, Kylie Jenner.

Msanii huyo amedai ataendelea kumpenda kwa kuwa alimzoea, lakini kwa sasa atakuwa kama rafiki yake wa kawaida na anaweza kumsaidia kama atahitaji msaada wake.

Akihojiwa na Big Boy TV, Tyga alisema Kylie alianza kubadilika tabia na alijaribu kumweka sawa lakini hali iliendelea kuwa hivyo japokuwa walikuwa wanaonekana wanapendana sana.

“Uhusiano unaonekana kuwa bora nje ya nyumba lakini ndani kuna mambo mengi yanatokea ila ni siri kati ya wahusika wenyewe.

Ni kweli nilikuwa naishi vizuri na Kylie lakini kuna baadhi ya mambo tulikuwa tunapishana, lakini nilikuwa tayari kumfanyia lolote katika maisha yake ila ndio hivyo tena kwa sasa hakuna la ziada kilichobaki ni kuwa marafiki wa kawaida,” alisema Tyga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles