25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Nick Cannon awalilia watoto wake

CannonNEW YORK, MAREKANI

RAPA Nick Cannon, amewalilia watoto wake aliozaa na msanii mwenzake, Mariah Carey, baada ya mrembo huyo kushinda kesi ya kukaa na watoto hao.

Cannon na Mariah walifunga ndoa mwaka 2008 na waliachana mwaka 2015 baada ya kupata watoto hao wawili mapacha, Monroe na Moroccan ambao walizaliwa Aprili 30, 2011.

Baada ya kuachana wawili hao walifikishana mahakamani kwa ajili ya haki ya kulea watoto hao na Mariah alishinda.

Kutokana na hali hiyo, Cannon ameamua kutunga wimbo kwa ajili ya kuwaaga watoto hao aliouita ‘Kwa heri wanangu’.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, msanii huyo ameandika namna anavyoumizwa na hukumu hiyo.

“Siwezi kuwa tena na wanangu, lakini nitawakumbuka sana kwa kuwa sijakaa na nyinyi, nakuwa na wakati mgumu kila nikiusikiliza wimbo wangu mpya, ila nawatakia maisha mema ipo siku tutakutana na kuwa pamoja,” aliandika Cannon.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles