25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Twanga ndani ya Mango Garden Aprili 16

Asha 2NA ASIFIWE GEORGE

BENDI ya muziki wa dansi ya Africans Stars ‘Twanga Pepeta’, inatarajia kukutanisha wanamuziki na wadau wa muziki wao katika onyesho lake litakalofanyika Ukumbi wa Mango Garden, Aprili 16 mwaka huu.

Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka, alisema onyesho hilo la ‘Usiku wa Pongezi’ na nyimbo zote za bendi hiyo zitakapigwa kwa kuwa ni la bendi hiyo tu na wadau wake.

“Lengo la onyesho hilo ni kuwakutanisha wadau wa Twanga ambao walikuwa wakikutana zamani na wapenzi wa muziki wao wa sasa ili waione bendi yao, waisikilize na waishauri kutokana na changamoto walizonazo.

“Pia katika onyesho hilo tutawakumbuka wanamuziki na wadau wa bendi hiyo waliotangulia mbele za haki kwa kusimama kwa dakika moja ili kuwaenzi na kuwaombea walipo wawe sehemu salama,” alimaliza Asha Baraka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles