P. Diddy kulirudisha kundi la Bad Boys

0
895

P.DiddNEW YORK, MAREKANI

MKALI wa rapu nchini Marekani ambaye ni mkurugenzi wa kundi la Bad Boys, P. Diddy, amedai anataka kulirudisha kundi hilo na kufanya shoo ya pamoja kwa ajili ya kumkumbuka nyota wa muziki huo, Notorious B.I.G. ambaye alifariki 1997.

Shoo hiyo inatarajiwa kufanyika Mei 21 ukumbi wa Brooklyn Barclays Arena, siku ambayo B.I.G alizaliwa, ambapo angetimiza miaka 44.

Mara ya mwisho kundi la Bad Boy kufanya onyesho la pamoja ilikuwa mwaka jana kwenye tuzo za Black Entertainment Television (BET).

“Hii itakuwa shoo ya kihistoria katika historia ya muziki wa hip hop ambapo wasanii wenye majina makubwa akiwemo Faith Evans, Lil Kim, Mase, 112, The Lox, Total, Frenc Montana na Mario Winans, wakati huo Jay Z na Mary J Blige wamealikwa,” alisema P. Diddy.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here