24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Khloe: Pombe itatenganisha uhusiano wetu

Khloe_KardashianNEW YORK, MAREKANI

BAADA ya nyota wa zamani wa mchezo wa kikapu nchini Marekani, Lamar Odom, kuendelea na ulevi wa pombe, mpenzi wake, Khloe Kardashian, amedai uhusiano huo utavunjika kutokana na pombe.

Oktoba mwaka jana, Odom alikimbizwa hospitali na kulazwa kutokana na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na pombe kupita kiasi, hivyo baada ya kutoka katika hospitali hiyo madaktari walimshauri aachane na ulevi huo lakini wiki iliyopita alionekana akirudia ulevi huo.

Khloe amedai anampenda sana Odom, lakini anaamini pombe zitamsababishia kifo mpenzi wake huyo na kuwa mwisho wa uhusiano wao.

“Odom ananiumiza kichwa, hospitali aliambiwa asinywe pombe lakini ameanza tena, hii inanipa wakati mgumu nikiamini kwamba kifo chake kitatokana na pombe, sina mpango wa kuachana naye lakini pombe inaweza kututenganisha kwa kupoteza maisha,” alieleza Khloe.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles