24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

TUNDU LISSU: NINAITWA MGONJWA WA MIUJIZA


Asha Bani na Nora Damian-DAR ES SALAAM

KITENDO cha Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, kupigwa risasi 17 mwilini, lakini akaendelea kuwa hai hadi leo, kimetafsiriwa na madaktari wanaomtibu kuwa ni muujiza unaoishi.

Hayo yalibainishwa na Lissu mwenyewe katika mahojiano maalumu na Kituo cha runinga cha Azam jana, kuhusu masuala mbalimbali tangu alipopigwa risasai nje ya nyumba yake mjini Dodoma, Septemba 7 mwaka jana na maendeleo ya matibabu yake kwa ujumla.

Katika mahojiano hayo, Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) alisema:

“Asubuhi daktari wangu anakuja kuniamsha kunifanyisha mazoezi, wamesema nitatembea tu kwani kutokana na maumivu na majeraha niliyoyapata mimi ni kama muujiza, wananiita mgonjwa wa miujiza unaoishi.

“Madaktari wangu wamesema hakuna kizuizi chochote cha matibabu kitakachozuia mimi kutembea. Wamesema  nitasimama, nitatembea, mapambano bado yanaendelea. Narekebisha kwanza mwili ukae sawa, maneno yapo sawa sawa.”

Lissu aliwashukuru pia madaktari wa hospitali hiyo kwa kumuhudumia vizuri na anafikiri hakuna hospitali nyingine inayoweza kufanana nayo katika Afrika ya Mashariki kwa ubora wake.

Katika mahojiano hayo, Lissu alielezea maumivu makali aliyoyapata baada ya kuzinduka hospitalini siku saba baada ya kupigwa risasi.

Aidha katika simulizi hiyo, pia alielezea namna risasi mbalimbali zilivyo………………………………..

Kwa habari zaidi usikose kununua nakala yako ya MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles