Timu ya Tumaini imetwaa ubingwa wa mashindano ya mtaani ya Meridian Bet street soccer bonanza yaliyofanyika leo Jumamosi kwenye uwanja wa Mwembeyanga, Temeke.
Bonanza hilo lililoudhuliwa na mkuu wa kituo cha Mwembeyanga, msaidizi wa polisi Cathbert Christopher kwa niaba ya mkuu wa kituo cha Chang’ombe, ASP Mohammed lilishirikisha timu nne likipigwa kwa udhamini wa kampuni ya michezo ya kubashiri matokeo ya Meridian Bet ambao wametoa vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu zote.
Twaha Mohammed wa kitengo cha masoko wa Meridian Bet amesema bonanza hilo ni la pili kufanywa na kampuni yao katika muendelezo wa ‘events’ za Street Soccer Bonanza.
Amesema utaratibu wa timu kushiriki ni ule ule kwa mashabiki kupendekeza majina ya timu wanazotamani zishiriki bonanza hilo na kupigiwa kura kwenye mitandao ya kijamii ya Meridian Bet.
Awali mkuu wa kituo cha Mwembeyanga, msaidizi wa polisi, Cathbert Christopher alisema bonanza hilo linasaidia kuwakutanisha watu mbalimbali katika matukio ya kimichezo na hata kupunguza uhalifu.
“Michezo ni moja ya vyao vikubwa vinavyosaidia kupunguza uharifu kwa kiasi kikubwa, hivyo hiki kinachofanywa na Meridian Bet ni sehemu ya harakati hizo,” amesema.
Katika bonanza hilo, timu ya Tumaini ilitawazwa kuwa bingwa kwa kuwachapa bao 1-0 wapinzani wao, timu ya Movement katika mchezo mkali wa fainali uliokuwa na upinzani wa hali ya juu.
Bao la mapema la Hamad Abdallah lilitosha kuipa ubingwa Tumaini, licha ya Movement kupambana kutaka kusawazisha, ngome ya ulinzi ya Tumaini ilikuwa makini kuondosha hatari.
Wisdom FC ilimaliza ya ya tatu kwa kuichapa Bonyokwa mabao 5-1 kwenye mechi iliyokuwa ya upande mmoja.
Shujaa wa Wisdom alikuwa Hassan Said aliyepiga ‘hat trick’ na kuongeza bao jingine hivyo kumaliza mechi hiyo akiwa amepachika mabao matatu, jingine likifungwa na Athuman Iddi wakati la kufutia machozi la Bonyokwa likifungwa na Ismail Ngasumo.