27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Musoma vijijini wafikishiwa maji ya bomba majumbani

Na Shomari Binda, Musoma

WANANCHI wa jimbo la Musoma vijijini wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwafikishia huduma ya maji hadi majumbani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mtanzania Digital katika vijiji vya Bulinga, Bukima na Wanyere, wamesema kwa sasa wanapata maji wakiwa nyumbani kwa wakati wote.

Wamesema kipindi cha nyuma wamekuwa na shida kubwa ya maji na kuyafata umbali mrefu nyakati za usiku.

Mkazi wa Kijiji cha Bulinga, Mgesi Kuboja amesema ameunganishiwa maji ya bomba nyumbani ambayo ni safi na salama na yanatoka wakati wote.

Amesema maji kwa sasa sio shida tena na kuishukuru serikali pamoja na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini,Profesa Sospeter Muhongo kwa kuwafikishia maji.

Msimamizi wa mradi wa maji wa Bulinga/Bujaga, Daniel Kulwa, amesema wananchi zaidi ya 70 tayari wamefikishiwa maji ya bomba nyumbani na vituo 79 vinatoa maji.

“Tunasimamua mradi vizuri na wananchi wanapata maji wakati wote na tunaishukuru serikali kwa hili la kumtua mama ndoo kichwani,” amesema Daniel.

Kwa upande wake, Masatu Mfungo, wa Kijiji cha Wanyere Kata ya Suguti, amesema kabla ya kuunganishiwa maji ya bomba nyumbani walikuwa wakilazimika kuamka usiku kufata maji kisimani na kukwamisha shughuli nyingine za maendeleo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,573FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles