25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Tulia mgeni rasmi Miss Tanzania

Na JEREMIA ERNEST

NAIBU Spika wa Bunge, Tulia Ackson anatarajiwa kuwa mgeni wa heshima katika mashindano ya miss Tanzania Desemba 5 katika ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam.

Walimbwende takribani 20 kutoka kanda nane za nchi watachuana kuwania zawadi ya gari aina ya Subaru, pamoja na nafasi ya kushiriki mashindano ya dunia mwaka kesho.

Akizungumza na MTANZANIA DIGITAL mratibu wa shindano hilo hapa nchini, Basilla Mwanukuzi, amesema mwaka huu mgeni wa heshima atakuwa Mheshimiwa Tulia Akison.

“Mwaka huu tuna bahati kubwa katika tasnia ya urembo Naibu Spika Tulia Ackson amekubali kuwa mgeni rasmi hii ni ishara ya kuwa serekali yetu ipo pamoja na sisi katika kukuza shindano hili,” anasema Basilla.

Aliongeza kuwa warembo wanaoshiriki wanatarajiwa kuingia kambini Novemba 29 katika hoteli ya Serene Mbezi beach, pia tiketi za fainali ni 100,000, 65000, 50000 na 25000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles