27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Wagombea nafasi ya Mwenyekiti Kiteto hadharani

Na Mohamed Hamad

Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa kimeteua majina kuwania nafasi za Uenyekiti katika halmashauri za wilaya kwa ajili yakupigiwe kura.
Upande wa wilaya ya Kiteto mkoani Manyara majina mawili ya wanachama kati ya tisa yamepitishwa kuwania nafasi ya Uenyekiti wa halmashauri tayari kwa kupigiwa kura.

Majina hayo ni, Abdallah Bundallah na Lairumbe Mollel ambaye anatetea nafasi hiyo aliyohudumu kwa miaka mitano iliyopita.
Jumla ya madiwani tisa walijitokeza kuwania nafasi hiyo huku makamu wa mwenyekiti wakijitokea wanachama watatu na ambao utaratibubwao unaandaliwa.
Akitangaza majina hayo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Haphrey Polepole leo jijini Dar es Salaam amesema majina hayo ndiyo yatakayopigiwa kura na madiwani katika halmashauri zao.
Baadhi ya wananchi wilayani Kiteto wamesema wajumbe watakaopiga kura wanapaswa kuwa makini kumpata kiongozi mwenye maslahi mapana na wananchi wa Kiteto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles