27.4 C
Dar es Salaam
Thursday, December 9, 2021

Tuchel meno kuiua Juventus

TURIN, Italia

MKUU wa benchi la ufundi la Chelsea, Thomas Tuchel, amesema vijana wake walitandaza soka la kiwango cha juu kuimaliza Juventus kwa kichapo cha mabao 4-0, mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa usiku wa jana.

Huku matokeo hayo yakiivusha Chelsea, Juve waliharibiwa siku kwa mabao ya Trevoh Chalobah, Reece James, Callum Hudson-Odoi na Timo Werner.

“… Ni ngumu kutengeneza nafasi na kufunga hapo hapo lakini tulifanya hivyo. Ni kiwango bora sana na matokeo mazuri pia,” amesema Tuchel.

Blues wamebakiza mchezo mmoja wa hatua ya makundi ya michuano hii, ambapo watasafiri kueleka Urusi iliko Zenit St Petersburg.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,672FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles