29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

TSC: Walimu 1,795 wamekiuka maadili

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

TUME ya Watumishi wa Walimu nchini (TSC) imesema kuwa jumla ya Walimu 1,795 wamebainika kutenda makosa matano ya ukiukaji wa maadili katika kipindi cha kuanzia Julai 2020 hadi Septemba 2021.

Makosa hayo ni utoro, kughushi vyeti, kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi, ukaidi na ulevi.

Tume hiyo imesema mashauri yao yaliamuliwa kwa asilimia 57.1 kwa kufukuzwa kazi huku asilimia 5.5 wakikosekana na hatia na kuachiwa huru.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Jumatano Desemba 29,2021 Mwenyekiti wa Tume hiyo, Profesa Willy Komba, amesema jumla ya walimu 1,795 waliobainika kutenda makosa matano ya ukiukaji wa maadili katika kipindi cha kuanzia Julai 2020 hadi Septemba 2021.

Amesema makosa waliyoshtakiwa nayo katika kipindi hicho ni pamoja na utoro ambao uliongoza kwa asilimia 51.9, kugushi vyeti asilimia 25.7, kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi kwa asilimia 11.8, ukaidi asilimia 6.3 pamoja  na ulevi ambao ni asilimia  4.4.

Prof. Komba amezitaja adhabu nyingine walizokumbana nazo walimu hao kuwa ni pamoja na karipio, kushushwa daraja, kupunguzwa mishahara, kuonywa na kulipa fidia.

Aidha, Mwenyekiti huyo ametoa wito kwa walimu kuhakikisha wanazingatia suala zima la maadili kwakuwa mfano wa kuigwa na jamii ikiwa ni pamoja na kuwafundisha wanafunzi suala zima la maadili katika kumlea mwanafunzi sio kuwaachia viongozi wa dini pekee.

“Elimu inaendana na maadili kusoma sio lazima kuelimika, kuelimika ni kuwa bora kiakili na mahusiano,tunashughudia madarasani walimu wengi wanafundisha maarifa na kusahau kufundisha maadili nawakumbusha kazi ya kuwakumbusha watoto maadili ni ya walimu,”amesema.

Vilevile, Profesa Komba amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na kuwajali walimu kutokana na kupandishwa vyeo hususan wale waliokuwa na sifa za kupanda madaraja wote walipandishwa madaraja.

Kuhusiana na ujenzi madarasa yaliyojengwa kutoka na fedha za Uviko-19 ameipongeza Serikali kwa ujenzi huo huku akidai utaendana na sera ya kukuza elimu nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles