25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Muhimbili wafunguka mbele ya Waziri Gwajima

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wananchi na wazazi wanaopata huduma kwenye kliniki ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamemuomba Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuongezewa wataalam wa huduma ya mishipa ya ubongo.

Wakizungumza mbele ya Waziri wa Afya, Dk. Dorothy Gwajima, leo Jumatano Desemba 29, 2021 mara baada kufanya ziara ya kutembelea kliniki ya watoto kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, na kuzungumza na wananchi na watoa huduma kisha kupokea maoni ya wazazi aliwaokuta wakipata huduma ndani ya kitengo hicho.

Wazazi hao wamemuomba yafanyike maboresho kwenye eneo la huduma za vyoo kwa ajili ya kuwasitiri watoto wadogo, kuwekewa feni ili kupunguza joto kwa watoto wadogo, kuongezewa mabenchi ya kukalia.

“Mheshimiwa tunaomba kuongezwa kwa wataalam wa huduma ya mishipa ya ubongo kwani uhitaji mkubwa,” amesema mmoja ya wananchi hao.

Kitengo hicho cha Mishipa ya fahamu pamoja na Ubongo, takwimu zinaonesha kinahudumia hadi Watoto 80 kwa siku, Idadi ambayo ni kubwa ikilinganishwa na Idadi ya Mabingwa waliopo kwa sasa.

Akijibu maswali ya wananchi na wazazi hao Dk. Gwajima amesema ameyapokea maoni na mapendekezo yaliyotolewa na kuahidi kuyafanyia kazi.

“Ndugu zangu nimewasikia, uzuri hapa tupo na Mkurugezi anawasikia pia, lakini kama haitoshi, naomba niwape namba yangu ya kunitumia ujumbe mfupi, hii sio kwa ajili ya kupiga, niandikie ujumbe, tushauri nini tuweze kuboresha, kwa kutumia wataalam wetu tutachukua maoni yenu na tutayafanyia kazi,” amesema Dk. Gwajima.

Katika hatua nyingine, Waziri Gwajima amemuelekeza Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufanyie kazi maboresho ambayo wananchi waliomba kuboreshewa, sambamba nakuendelea kuchukua maoni zaidi kwenye maeneo mbalimbali ambayo yatawasilishwa na wananchi ili huduma ziweze kuboreshwa.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Prof Laurence Museru aliahidi kuyafanyia kazi maboresho hayo, ambayo wananchi waliwasilisha ili kuweza kutatuliwa sambamba na kuongeza wataalam Bingwa wa masuala ya matatizo ya watoto ya Ubongo Pamoja na mishipa ya fahamu.

“Mheshimiwa Waziri tumeyachukua haya ambayo wananchi wamewasilisha mbele yako, lakini mkakati mwingine tulionao ni kuongeza wataalam wabobezi kwa kuwapeleka shule ili wakihitimu waweze kusaidiana na hawa waliopo na kuondoa kabisa mapungufu haya ama kuyapunguza kwa asilimia kubwa,” amesema Prof. Mseru.

Awali, kabla ya kuwatembelea na kuzungumza wananchi hao waliofika kwa ajili ya huduma za kitabibu, Waziri Dk. Gwajima, alifanya kikao cha pamoja na Uongozi wa Hospitali hiyo kwa lengo la kukumbusha wajibu na kuweka mikakati ya uboreshaji wa huduma zinazo tolewa na Hospitali hiyo ya Taifa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles