28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Trump na Biden wapiga kampeni katika uchaguzi wa Seneti Georgia

Georgia, Marekani

Uchaguzi wa duru ya pili wa viti viwili vya seneti huko katika jimbo la Georgia unafanyika Jumanne hii na utaamua ikiwa Warepublican au Wademokrat watachukua udhibiti kwenye baraza la Seneti la Marekani na kubadili kwa kasi utekelezaji wa sera katika nusu ya kwanza ya muhula wa miaka minne wa Rais mteule Joe Biden katika Ikulu ya Marekani.

Huku uchaguzi ukiwa na umuhimu mkubwa wote, Biden na Rais anayemaliza muda wake, Donald Trump wamefanya mikutano ya kampeni ya dakika za mwisho katika jimbo hilo Jumatatu.

Hata wakati Trump akiendelea na malalamiko yake dhidi ya maafisa wa uchaguzi wa Georgia kwa kukataa kubadili matokeo ya uchaguzi ambayo alishindwa kwa kura chache na Joe Biden katika jimbo hilo katika uchaguzi wa Novemba 3.

Biden amefanya kampeni huko Atlanta, jiji kubwa zaidi la Georgia, kwa Wademokrat wawili, Jon Ossoff, mtayarishaji wa filam , na Mchungaji Raphael Warnock, mchungaji wa kanisa la Baptist.

Wakati huo huo, Trump amefanya kampeni katika eneo kubwa la Warepublican huko Dalton kaskazini mwa jimbo hilo ajili ya, Seneta David Perdue, ambaye wakati fulani alikuwa mfanyabiashara mkubwa anayekabiliana na Ossoff, na kwa Seneta Kelly Loeffler, mmoja wa seneta tajiri zaidi Marekani ambaye anakabiliana na mchungaji Warnock.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles