26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Kidato cha kwanza 350 wakosa nafasi Moshi

Safina Sarwatt, Moshi

Jumla ya wanafunzi 350 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule mbalimbali halmashauri ya wilaya ya Moshi vijijini wamekosa nafasi kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa.

Akizungumza wakati akipokea msaada wa mifuko 100 ya saruji iliyotolewa na mbunge wa jimbo la Moshi vijijini, Prof Patrick Ndakidemi leo Januari 6, 2021, Ofisa elimu sekondari wilaya ya Moshi, Juma Tukosa amesema jumla ya wanafunzi waliofaulu ni kidato cha ni 7,925, kati ya hao wanafunzi 350 hawajachaguliwa kutokana na upungufu wa madarasa.

Amesema kuwa kutokana na upungufu halmashauri tayari imeshaanza kuchukua hatua ili kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanaanza masomo mapema.

“Halmashauri tayari imeshatoa zaidi ya milioni 30 kwa ajili ya matundu ya vyoo pamoja na ukarabati mdogo mdogo wa miundombinu ya madarasa,”amesema.

Amesema halmashauri hiyo inajumla ya shule za sekondari 98 kati hizo za serikali ni 56 na za binafsi ni39.

Akitoa msaada huo wa mfuko ya saruji 100 kwa shule ya sekondari ya Mpirani na shule ya sekondari Mabogini, Prof. Ndakidemi amewataka wadau kuunganisha nguvu ili kuhakikisha madarasa hayo yanakamilika kwa wakati na wanafunzi wanaanza masomo.

“Nimeona ni changia katika ujenzi wa madarasa saba katika shule ya Mabogini na shule ya sekondari Mpirani lengo nikuhakikisha kwamba wanafunzi 350 walio kosa nafasi wanaanza masomo yao mapema,” amesema.

Aidha, ametoa mifuko ya saruji 60 kwa shule ya sekondari Mpirani kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili ambapo uhitaji ni madasara 8 na mifuko 40 kwa shule sekondari Mabogini uhitaji madarasa matatu.

Diwani wa kata ya Mabogin, Dk. Bibiana Masawe amesema kata hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa pamoja na upumbufu wa matundu ya vyoo kulingana na idadi ya wanafunzi walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles