26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge kuingia bungeni na bunduki

Washington, Marekani

Mbunge mmoja wa Chama cha Republican cha Rais Donald Trump, Lauren Boebert ameahidi kutembea na silaha aina ya bunduki wazi mitaani.

Mbunge huyo mpya mwanamke ameahidi kutembea na bunduki wakati wa muhula wake wa kwanza huko Washington DC.

Katika video iliyotolewa Jumapili, mbunge wa Republican Lauren anaonekana akiweka bunduki yake ya mkononi risasi kabla ya kuanza kutembea nayo mjini.

“Nitabeba bunduki yangu nikiwa Washington DC na bungeni pia,” amesema katika video ambayo imetazamwa na watu zaidi ya mara milioni mbili.

Lakini Mkuu wa polisi amesema anapanga kuzungumza na mbunge huyo kuhusu sheria kali za kubeba bunduki.

Mbunge huyo ni mmiliki wa mgahawa unaojulikana kama ‘Shooters Grill mjini Rifle Colorado, ambako watu huamasishwa kubeba silaha zao wazi kwa sababu kisheria huko, inaruhusiwa.

Suala la haki ya kumiliki bunduki ilikuwa sehemu ya msingi wakati wa kampeni yake katika uchaguzi uliofanyika Novemba 3.

“Hata kama sasa hivi nafanyakazi katika moja ya miji huru Marekani, siwezi kutupilia mbali haki yangu

“Kama Mwanamke Mwenye urefu wa futi tano, na uzito wa kilogramu 45, nina chagua kujilinda mweyewe kwasababu mimi ndio mlinzi mzuri kwangu binafsi,” amesema mbunge huyo kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Hata hivyo polisi wamejibu kwa haraka huku mkuu wa polisi Washington, DC Robert Contee III akiwaambia wanahabari kuwa:

“Mbunge atakabiliwa na adhabu ile ile kama mtu mwingine yeyote anayepatikana akiwa amebeba silaha katika mji wa DC,”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles