29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP ‘KUMTEUA’ MSHIRIKA WA PUTIN MAMBO YA NJE

WASHINGTON, MAREKANI


donald-trumpRAIS mteule Donald Trump huenda akamtangaza ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya mafuta ya Exxon Mobil mwenye uhusiano wa karibu na Rais wa Urusi Vladimir Putin kuwa mwanadiplomasia namba moja  Marekani.

Jina la Ofisa Mkuu Mtendaji huyo wa Exxon, Rex Tillerson lilijitokeza Ijumaa iliyopita kama mtu anayefaa zaidi miongoni mwa wanaopewa nafasi ya uwaziri wa mambo ya nje wa Marekani, kwa mujibu wa timu yake ya mpito.

Vyanzo viwili vya habari katika timu hiyo, vimeripoti kuwa Tillerson alitarajiwa kukutana na Trump na atatangazwa kushika wadhifa huo.

Awali Rais mteule alifanya mahojiano na mgombea urais wa mwaka 2012 kupitia chma chake cha Republican, Mitt Romney mara mbili ikiwamo kula naye chakua cha usiku.

Lakini inasemekana sasa Trump ameachana na mpango wa kumpa wadhifa huo gavana huyo wa Massachusetts.

Tillerson anapewa nafasi kubwa baada ya Meya wa zamani wa New York, Rudy Giuliani kujitoa rasmi katika orodha ya wanaofikiriwa kushika wadhifa huo.

Kujitoa kwa Giuliani kumekuja baada ya uchunguzi wa kina kuhusu shughuli zake za kibiashara ng’ambo, hali ambayo timu ya Trump inaona itasababisha mgongano wa maslahi.

Hata hivyo, iwapo Tillerson atateuliwa suala la mgongano wa maslahi litakuwepo kutokana na ukaribu wake na Putin pamoja na shughuli za Exxon Mobil katika nchi zaidi ya 50 katika mabara sita duniani.

Mwaka 2011, Exxon Mobil ilisaini mkataba na Rosneft, kampuni kubwa ya taifa ya mafuta Urusi kwa ubia unaoshirikisha masuala ya utafiti na uzalishaji mafuta.

Mwaka 2013, Rais Vladimir Putin alitoa tuzo ya juu kabisa ya urafiki kwa Tillerson, ambaye ni mpinzani mkubwa dhidi ya vikwazo vya Marekani kwa Urusi.

Iwapo Trump atamteua Tillerson utaonesha dhamira ya bilionea huyo kuimarisha uhusiano wa utawala wa Putin, kama kama walivyoahidi baada ya kusifiana mara kwa mara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles