27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

MAGARI 13 YAGONGANA, YAUA 42 KENYA

NAIROBI, KENYA


joseph-nkaisseryWATU 42 wamekufa baada ya magari 13 yakiwamo lori lililosheheni mafuta pamoja na gari lililokuwa na mitungi ya gesi kugongana katika barabara kuu inayounganisha Kenya na Uganda usiku wa kuamkia jana.

Kwa mujibu wa Naibu Kamanda Mkuu wa Jimbo la Nakuru Isaaca Masinde, ajali hiyo ilitokea kaskazini mwa mji wa Naivasha katika eneo la Karai linalojulikana kwa shughuli nyingi.

Afisa mmoja mjini Naivasha amesema watu 50 wameungua vibaya na wanatibiwa hospitali,wanane kati yao wako mahatuti.

Akihutubia wanahabari jana, Waziri wa Mambo ya Ndani, Joseph Nkaissery amesema miongoni mwa waliokufa ni polisi 11 wa kikosi cha Recce kinachomlinda rais na watu wengine mashuhuri.

Nkaisssery alisema kuwa si gari la kusafirisha mafuta lililolipuka bali aina ya Canter lililokuwa na mitungi ya gesi inayoshika moto kwa haraka.

Mitungi hiyo ilikuwa ikisafirishwa kutoka Mombasa kwenda Kampala, Uganda,.

Mmoja wa mashuhuda alisema baada ya mgongano, magari kadhaa yalishika moto na kuanza kuteketea huku watu wengi waliofika eneo la ajali hiyo kushuhudia kilichotokea nao wakijikuta wakikumbwa na moto huo kutokana na mlipuko na kuanza kuteketea.

Polisi wanachunguza chanzo cha ajali hiyo. Kuna ripoti kuwa gari aina ya Canter iligonga tuta la barabarani na kisha kuyagonga magari yaliyokuwa yakitokea mbele kabla ya kulipuka.

Miongoni mwa magari yaliyoteketea ni basi moja la matatu lililokuwa na abiria 14, ambao wote wanahofiwa kufa.

Ajali hiyo mbaya imetokea nchini Kenya, wakati ambao madaktari na wauguzi walikuwa wakiendelea na mgomo ambao umeripotiwa kumalizika jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles