27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Trump amsifu Saddam

Donald Trump
Donald Trump

NORTH CAROLINA, MAREKANI

MGOMBEA urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amemsifu kiongozi wa zamani wa Irak, Saddam Hussein akisema aliwakabili vyema magaidi.

Trump alimzungumza kiongozi huyo aliyenyongwa Desemba 2006 wakati akihutubia mkutano wa kampeni jimboni hapa juzi.

“Saddam Hussein alikuwa mbaya, kweli? Lakini mnafahamu ni jambo gani aliweza kulifanya vyema? Aliwaua magaidi. Alifanya hivyo kwa ufanisi,” Trump alisema.

“Hakuwasomea haki zao, hawakunena lolote. Walikuwa magaidi, kwake, mambo yao kwisha!.”

Trump aliwahi kukaririwa akisema ulimwengu ungekuwa ‘asilimia 100 bora kuliko sasa’ iwapo viongozi wa kiimla kama Saddam Hussein na Muammar Gaddafi wa Libya wangelikuwa bado madarakani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles