Baby J: Siringi mnanichukia bure

0
1103
Jamila Abdallah ‘Baby J’
Jamila Abdallah  ‘Baby J’
Jamila Abdallah ‘Baby J’

NA THERESIA GASPER

MMOJA wa wasanii wa Zanzibar watakaotumbuiza katika Tamasha la Filamu la Kimataifa (ZIFF), Jamila Abdallah  ‘Baby J’, amewataka wanaomchukia na kudhani kwamba anadharau wabadilishe mitazamo yao kwa kuwa yeye ni mtu wa kawaida mwenye tabia za kuzungumza na kujichanganya na watu wa rika zote.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Baby J alisema anapenda kushirikiana na amejiwekea tabia za kuzungumza na kila mtu tofauti na baadhi ya watu wanavyomtafsiri.

“Watu wengi wanaona wasanii huwa tunaringa au tunadharau kutokana na kazi zetu kitu ambacho kwangu si sahihi kwa kuwa napenda ushirikiano na kila mtu,” alisema.

Msanii huyo alisema mbali na kazi yake ya muziki vile vile amejikita katika biashara ya vipodozi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here