20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Christian Bella kupamba matembezi ya KCBL

Christian Bella
Christian Bella

NA MWANDISHI WETU,

MSANII wa muziki wa dansi, Christian Bella maarufu kama Mfalme wa Masauti, anatarajiwa kutoa burudani ya aina yake mjini Moshi wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (KCBL).

Akizungumza katika mahojiano maalumu, msanii huyo alisema yeye na bendi yake ya Malaika wamejiandaa vizuri na ana uhakika Moshi nzima itahamia katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU).

“Nawaomba wakazi wa Moshi wajitokeze kwa wingi kuiunga KCBL mkono katika matembezi haya ya hisani na baadaye tukutane katika Uwanja wa MoCu kwa burudani ya aina yake,” alisema.

Msanii huyu ambaye mwaka huu ametimiza miaka 10 wa muziki wake, anatamba na ‘Najuta’, ‘Nani kama mama’, ‘Nakuhitaji’, ‘Usilie’, ‘Msaliti na Hanitaki Tena’.

KCBL inaadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake na imetumia wiki hii kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho haya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles