24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

JPM aifumua awamu ya nne

RAIS Dk. John Magufuli
RAIS Dk. John Magufuli

*Asafisha wakurugenzi wa halmashauri 120

*Abakisha wa zamani 65, mbunge naye ateuliwa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

RAIS Dk. John Magufuli, amefumua uteuzi wa wateule wa Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete huku akiibua sura mpya katika nafasi mbalimbali za uongozi.

Hatua ya kiongozi huyo inaelezwa kuwa ni makakati wa kuisuka Serikali yake kwa kuibua watendaji wapya ambao hawana majina makubwa.

Hadi sasa kiongozi huyo wa nchi ameteua wakuu wa mikoa 26, ambapo kati yao wapya ni 13  na wengine 13 akiwaacha kuendelea na wadhifa.

Siku moja baada ya uteuzi huo, Rais Dk. Magufuli, aliteua makatibu tawala wa mikoa 26, ambapo kati ya hao 10 ni wapya huku 13 wa zamani akiwabakisha na wawili aliwabadili vituo vya kazi.

Juni 25, mwaka huu Rais Magufuli, aliteua tena wakuu wa wilaya 139, ambapo kati ya hao 101 ni wapya huku akiwabakisha wa zamani 38 tu.

Taarifa iliyotolewa jana na Ikulu jijini Dar es Salaam, ilieleza kuwa Rais Magufuli, amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji 5, Manispaa 21, Miji 22 na Wilaya (DC) 137 za Tanzania Bara.

Uteuzi huo ulitangazwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe,  ambapo kati ya wakurugenzi wote 185 walioteuliwa, 65 wametoka orodha ya wakurugenzi wa zamani na 120 ni wakurugenzi wapya.

Orodha ya wakurugenzi walioteuliwa kulingana na mikoa yao ni kama ifuatavyo;

ARUSHA

  1. Arusha Jiji       –      Athumani Kihamia
  2. Arusha DC        –      Wilson Charles
  3. Karatu DC        –      Banda Sonoko
  4. Longido DC     –      Jumaa Mhiwapijei
  5. Meru DC          –      Kazeri Japhet
  6. Monduli DC    –      Stephen Ulaya
  7. Ngorongoro DC    –      Raphael Siumbu

DAR ES SALAAM

  1. Dar es salaam Jiji –      Siporah Liana
  2. Kinondoni Manispaa –      Aron Kagurumjuli
  3. Temeke Manispaa –      Nassibu Mmbaga
  4. Ilala Manispaa –      Msongela Palela
  5. Kigamboni Manispaa –      Stephen Katemba
  6. Ubungo Manispaa –      Kayombo John

DODOMA

  1. Dodoma Manispaa -Wazi
  2. Kondoa DC –      Kibasa Mohamed
  3. Kondoa Mji –      Khalifa Mponda
  4. Mpwapwa DC –   Mohamed Maje
  5. Kongwa DC –      Mhandisi Laurent Izengo
  6. Chemba DC –      Semistatus Mashimba
  7. Chamwino DC –   Athuman Masasi
  8. Bahi DC              –     Rachel Chuwa

GEITA

  1. Bukombe DC –      Dionis Nyinga
  2. Chato DC –      Mhandisi Bahahari
  3. Geita DC –      Ally Kidwaka
  4. Geita Mji –      Modest Apolinaly
  5. Mbogwe DC –      Mahwago Elias Kayandabila
  6. Nyang’wale DC –      Carlos Gwamagobe

IRINGA

  1. Iringa Manispaa –      William Mafwele
  2. Mafinga Mji –      Saada Mwaruka
  3. Mufindi DC –      Riziki Shemdoe
  4. Iringa DC –      Robert Magunya
  5. Kilolo DC –      Aloyce Kwezi

KAGERA

  1. Biharamulo DC –      Wende Ng’ahala
  2. Bukoba DC –      Abdulaaziz Hussein
  3. Bukoba Manispaa –      Makonda Stephen
  4. Karagwe DC –      Godwin Kitonka
  5. Kyerwa DC –      Shedrack Mhagama
  6. Missenyi DC        –      Limbe Maurice
  7. Muleba DC –      Emmanuel Shelembi Luponya
  8. Ngara DC –      Aidan Bahama

   KATAVI

  1. Mlele DC –      Alex Kagunze
  2. Mpimbwe DC –      Erasto Kiwale
  3. Mpanda DC –      Ngalinda Ahmada
  4. Mpanda Manispaa –      Michael Nzyungu
  5. Nsimbo DC –      Joachim Nchunda

 KIGOMA

  1. Buhigwe DC –      Anosta  Nyamoga
  2. Kakonko DC        –      Lusubilo Mwakabibi
  3. Kasulu DC –      Godfrey Masekenya
  4. Kasulu Mji –      Fatina Laay
  5. Kigoma Ujiji – Manispaa -Judethadeus Mboya
  6. Kigoma DC –      Hanji Godigodi
  7. Kibondo DC        –      Shelembi Manolo
  8. Uvinza DC –      Weja Ng’olo

 KILIMANJARO

  1. Manispaa ya Moshi –      Michael Mwandezi
  2. Hai DC                –    Yohana Sintoo
  3. Siha DC                –    Valerian Juwal
  4. Same DC         –      Shija Anaclaire
  5. Mwanga DC         –     Golden Mgonzo
  6. Rombo DC         –     Magreth John
  7. Moshi DC         –     Emalieza Chilemeji

LINDI

  1. Kilwa DC –      Bugingo Zabron
  2. Lindi DC –      Samwel Gunzar
  3. Lindi Manispaa –      Jomaary Satura
  4. Liwale DC –      Justine Monko
  5. Nachingwea DC –      Bakari Mohamed Bakari
  6. Ruangwa DC        –      Andrea Chezue

 MANYARA

  1. Babati Mji –      Fortunatus Fwema
  2. Hanang DC –      Bryceson Kibasa
  3. Mbulu DC –      Festi Fwema
  4. Mbulu Mji –      Anna Mbogo
  5. Simanjiro DC        –      Yefred Myezi
  6. Kiteto DC –      Tamim Kambona
  7. Babati DC –      Hamis Malinga

 MARA

  1. Manispaa ya Musoma –      Fidelica Myovela
  2. Bunda DC –      Amos Kusaja
  3. Bunda Mji –      Janeth Mayanja
  4. Butiama DC –      Solomon Ngiliule
  5. Musoma DC        –      Flora Yongolo
  6. Serengeti DC        –      Juma Seph
  7. Rorya DC –      Charles Chacha
  8. Tarime DC –      Apoo Tindwa
  9. Tarime Mji –      Hidaya Usanga

MBEYA

  1. Busokelo DC        –      Eston Ngilangwa
  2. Chunya DC –      Sofia Kumbuli
  3. Kyela DC –      Mussa Mgata
  4. Mbarali DC –      Kivuma Msangi
  5. Mbeya DC –      Ameichiory Josephat
  6. Mbeya Jiji –      Zacharia Ntandu
  7. Rungwe DC –      Loema Peter

SONGWE

  1. Momba DC –      Adrian Jungu
  2. Tunduma Mji        –      Valery Kwemba
  3. Mbozi DC –      Edna Mwaigomole
  4. Ileje DC        –      Haji Mnasi
  5. Songwe DC –      Elias Nawela

MOROGORO

  1. Gairo DC –      Agnes Mkandya
  2. Kilombero DC –      Dennis Londo
  3. Ifakara Mji –      Francis  Ndulane
  4. Kilosa DC –      Kessy Mkambala
  5. Morogoro DC –      Sudi Mpili
  6. Morogoro Manispaa –      John Magalula
  7. Mvomero DC –      Florent Kyombo
  8. Ulanga DC –      Audax Rukonge
  9. Malinyi DC –      Marcelin Ndimbwa

MTWARA

  1. Mtwara DC –      Omari Kipanga
  2. Mtwara Mikindani Manispaa -Beatrice Kwai
  3. Masasi Mji –      Gimbana Ntayo
  4. Masasi DC –      Mkwazu  Changwa
  5. Nanyumbu DC –      Hamis Dambaya
  6. Newala DC –      Mussa Chimae
  7. Newala Mji –      Andrew Mgaya
  8. Tandahimba DC –      Said Msomoka
  9. Nanyamba Mji –      Oscar Ng’itu

MWANZA

  1. Mwanza Jiji –      Kiomoni Kiburwa
  2. Ilemela Manispaa –      John Wanga
  3. Kwimba DC –      Pendo Malabeja
  4. Magu DC –      Lutengano Mwalwiba
  5. Misungwi DC –      Eliud Mwaiteleke
  6. Ukerewe DC        –      Tumaini Shija
  7. Buchosa DC –      Crispian Luanda
  8. Sengerema DC –      Magesa Boniphace

NJOMBE

  1. Njombe Mji –      Iluminata Mwenda
  2. Makambako Mji –      Paul Malala
  3. Makete DC –      Francis Namaumbo
  4. Njombe DC –      Monica Kwiluhya
  5. Ludewa DC –      Ng’wilabuzu Ludigija
  6. Wanging’ombe DC –      Amina Kiwanuka

PWANI

  1. Bagamoyo DC –      Azimina Mbilinyi
  2. Chalinze DC        –      Edes Lukoa
  3. Kibaha DC –      Tatu Kikwete
  4. Kibaha Mji –      Jenifer Omolo
  5. Kisarawe DC        –      Mussa  Gama
  6. Mafia DC –      Erick Mapunda
  7. Mkuranga DC –      Mshamu Munde
  8. Kibiti DC –      Alvera Ndabagoye
  9. Rufiji DC –      Salum Rashid Salum

 RUKWA

  1. Kalambo DC        –     Simon Lyamubo
  2. Sumbawanga DC –     Nyangi Msemakweli
  3. Sumbawanga Manispaa -Hamid Njovu
  4. Nkasi DC –      Julius Kaondo

RUVUMA

  1. Mbinga DC –      Gumbo Samanditu Gumbo
  2. Mbinga Mji –      Robert Kadaso Mageni
  3. Namtumbo DC –      Christopher Michael Kilungu
  4. Nyasa DC –      Oscar Mbuzi
  5. Songea DC –      Simon Bulenganija
  6. Madaba DC –      Shafi Mpenda
  7. Tunduru DC        –      Abdallah Mussa
  8. Songea Manispaa –      Tina Sekambo

SHINYANGA

  1. Kishapu DC –      Stephen Magoiga
  2. Msalala DC –      Berege Simon
  3. Shinyanga DC –      Mark Malembeka
  4. Kahama Mji –      Anderson Msumba
  5. Shinyanga Manispaa –     Lewis Kalinjuna
  6. Ushetu DC –     Michael Matomola

SIMIYU

  1. Bariadi DC –      Abdallah Malela
  2. Bariadi Mji –      Melkizedek Humbe
  3. Itilima DC –      Mariano Manyingu
  4. Maswa DC –      Fredrick Sagamiko
  5. Busega DC –      Anderson Njiginya
  6. Meatu DC –      Said Manoza

 SINGIDA

  1. Ikungi DC –      Rustika Turuka
  2. Iramba DC –      Linno Mwageni
  3. Mkalama DC        –      Martin Mtanda
  4. Manyoni DC        –      Charles Fussi
  5. Itigi DC        –      Luhende Gerald
  6. Singida DC –      Rashid Mandoa
  7. Singida Manispaa –      Kizito Brava

  TABORA

  1. Igunga DC –      Revocatus Kuuli
  2. Kaliua DC –      John Pima
  3. Nzega DC –      Jacob Mtalitinya
  4. Nzega Mji –      Phillimon Magesa
  5. Sikonge DC –      Simon Ngatunga
  6. Tabora Manispaa –      Bosco Ndunguru
  7. Urambo DC –      Magreth Nakainga
  8. Tabora -Uyui        –      Hadija Makuani

 TANGA

  1. Tanga Jiji –                  Daudi Mayeji
  2. Korogwe DC        –      George Nyaronga
  3. Korogwe Mji        –      Jumanne Kiangoshauri
  4. Muheza DC          –      Luiza Mlelwa
  5. Handeni Mji        –     Keneth Haule
  6. Handeni DC        –      William Mafukwe
  7. Pangani DC         –      Sabas Chambasi
  8. Mkinga DC         –      Mkumbo Barnabas
  9. Bumbuli DC       –     Peter Nyalali
  10. Kilindi DC           –     Clemence Mwakasenda
  11. Lushoto DC         –    Kazimbaya Adeladius

Kutokana na uteuzi huo wateule wote wametakiwa kufika Ikulu Jijini Dar es Salaam Jumanne Julai 12, mwaka huu kwa ajili ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles