Ulinzi mkali Netanyahu akiwasili Rwanda

0
1158
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kushoto na Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kushoto na Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kushoto na Rais wa Rwanda Paul Kagame.

KIGALI, RWANDA

ULINZI mkali ulishuhudiwa jana katika mji mzima wa Kigali wakati Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwasili kwa ziara ya siku moja.

Wakati askari wakiwa wametanda kila kona ya jiji, barabara kuu zinazounganisha mji huo mkuu na uwanja wa ndege zilifungwa na kusababisha foleni na usumbufu mkubwa.

Netanyahu aliye ziara ya siku nne barani Afrika yuko hapa kwa saa chache ambapo pamoja na mambo mengine atatembelea kumbukumbu ya mauaji ya kimbari huko Gisozi na anatarajia kufanya mazungumzo na Rais Paul Kagame katika Kijiji cha Urugwiro.

Wakati akiwasili alikaribishwa na Kagame na kukagua gwaride la heshima uwanja wa ndege kabla ya kuelekea Gisozi anbako kuna mabaki ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Wawili hao walitarajia kufanya mkutano wa pamoja na wahabari kabla ya Netanyahu kuhitimisha ziara yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here