30.1 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Trump ampa wakati mgumu Hillary

1920

NA JUSTIN DAMIAN, NORTH CAROLINA

WIKI moja kabla ya uchaguzi wa Marekani kufanyika, mgombea urais bilionea kupitia Chama cha Republican hapa Marekani, Donald Trump, ameonekana kutoa upinzani mkali kwa mgombea wa Chama cha Democrat, Hillary Clinton, anayepewa nafasi kubwa ya kushinda.

Trump aliyekuwa akipewa nafasi finyu ya kushinda kiti cha urais, amemsogelea karibu mpinzani wake kwenye majimbo yenye ushindani mkali (swing states).

Wachambuzi wa siasa hapa Marekani, wanasema upepo umembadilikia Hillary kutokana na kashfa mpya ya matumizi ya barua pepe binafsi wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Hadi kufikia hivi sasa, jumla ya wapiga kura milioni 21 kati ya wapiga kura zaidi ya milioni 146 tayari wameshapiga kura zao.

Katika majimbo ambayo yanaweza kuamua nani atashinda kama vile Florida, Colorado na Nevada, karibu robo ya wapiga kura tayari wameshajitokeza kupiga kura, lakini kura zao zitahesabiwa baada ya uchaguzi.

Hata hivyo, wanachama wa Democrat wameonekana kujitokeza kwa wingi kuliko Republican katika sehemu zenye ushindani mkali kama hapa North Carolina, japokuwa tofauti ni ndogo.

Baadhi ya wanachama wa Hillary, wameamua kurudi kwa Trump kutokana na kashfa inayomkabili ya barua pepe ambayo mpaka sasa haijafahamika mwisho wake utakuwaje.

“Hatuwezi kuyumbishwa na kelele za kisiasa, Clinton aliuambia umati uliohudhuria mkutano wake wa hadhara uliofanyika Jumapili Florida na kuwakumbusha kuwa wakazi milioni 3 wa Florida tayari wameshapiga kura. “Lazima tubaki kwenye lengo letu la ushindi,” alisema.

Wakati kura za awali zikiendelea kuonyesha mafanikio kwa Hillary, kumekuwa na mabadiliko mwishoni mwa wiki ambapo Wamarekani wenye asili ya Afrika hapa North Carolina hawakujitokeza kwa wingi kama walivyofanya mwaka 2012.

Wamarekani weusi wamekuwa ni wapiga kura wazuri wa Democrat hapa North Carolina na kutoshiriki kwao ni pigo kwa chama hicho.

Mmoja wa wapiga kura, Craig Troman, aliliambia MTANZANIA kuwa ameamua kumpigia kura Trump kwa kuwa anaamini ataleta mabadiliko

Siwezi kumpigia Hillary kwa kuwa alionyesha udhaifu mkubwa wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje, nadhani hafai kuiongoza Marekani,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles