MEXICO CITY, MEXICO
MGOMBEA urais wa Chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump, amekubali mwaliko wa kumtembelea Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto.
Ikulu ya hapa imesema kwamba mipango ya kufanyika kwa mazungumzo ya faragha baina ya wawili hao inakaribia kukamilishwa.
Mkutano huo utafanyika muda mfupi kabla ya Trump kutoa hotuba kuhusu uhamiaji nchini Marekani.
Kwenye kampeni, Trump amewaeleza wahamiaji wa Mexico wanaoingia Marekani kama ‘wahalifu’ na ‘wabakaji.’
Kwa sababu hiyo, ameahidi kujenga ukuta kuwazuia wahamiaji hao kuingia nchini humo iwapo atachaguliwa kuwa rais.
Hata hivyo, Rais Pena Nieto pia ametoa mwaliko kwa mgombea urais wa chama cha Democratic, Hillary Clinton.