28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Pluijm: Yanga ni imara

Hans van der Pluijm.
Hans van der Pluijm.

NA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

BAADA ya kuanza kwa kishindo katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, amesema uimara wa kikosi ndio umechangia wachezaji kujiamini na kuendelea kuwa fiti uwanjani.

Yanga ambao wametetea taji la ubingwa wa ligi hiyo kwa misimu miwili mfululizo, ilianza msimu mpya kwa kasi baada ya Jumapili iliyopita kuichapa African Lyon mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kocha huyo raia wa Uholanzi, aliliambia MTANZANIA jana kuwa wachezaji wanajiamini uwanjani kutokana na mambo mengi hasa kama miili yao iko fiti na imeimarishwa kwenye mazoezi kwani hata akili zao zinakuwa zimetulia ili kufikia malengo.

Alisema pamoja na wachezaji kujikita kwenye mambo hayo muhimu katika kusaka ushindi, bado haamini kama uwezo wa timu uwanjani unaweza kubaki kwenye kiwango bora muda wote bila kufanyiwa maboresho kila wakati ili kuendana na ushindani uliopo.

Alieleza kuwa ushindi unatokana na motisha kwa wachezaji, jambo ambalo analifanyia kazi na kulipa kipaumbele kila mara wakati akitoa maelekezo kwenye mazoezi.

“Kama akili za wachezaji zimetulia lazima watafanya mambo mazuri uwanjani kutokana na kujiamini kwao, pia ninaamini ushindi unatokana na motisha wanayopata wachezaji katika kufikia malengo yaliyokusudiwa,” alisema Pluijm.

Aidha, Mholanzi huyo alisema jambo la msingi kwake ni kuhakikisha timu inajiandaa vizuri kwa kuitilia mkazo mechi inayofuata Ligi Kuu ili kuendeleza wimbi la ushindi huku akidai kwa sasa hawana muda wa kupoteza.

Kikosi cha Yanga kimerejesha makali yake Ligi Kuu baada ya kushindwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Yanga ilianza kushiriki mechi za kimataifa kwenye Klabu Bingwa Afrika lakini ikaondolewa hatua ya 16 bora na kuingia Kombe la Shirikisho ambapo ilifanikiwa kuingia hatua ya makundi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles