Na Safina Sarwatt, Moshi
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiasha kuhakikisha wanatumia mfumo rasmi wa stemp za kielectronic unaojulikana kama eTs ili kubaini uhalali wa stemp za bidhaa wanazoziuza na kwamba hatua hiyo itawawezesha pia kutambua bidhaa bandia.
Taarifa zaidi na .
Akizugumza wakati wa zoezi la utoaji elimu kwa wafanyabishara mjini Moshi mkoani Kilimanjaro leo Desemba 22, 2023 Meneja wa Mradi eTS kutoka TRA, Abihudi Tweve amesema kuwa ni vema wakatambua mfumo huo ambao utasaidia kubaini bidhaa bandia kwa urahisi.
Amesema kila mfanyabiashara atatakiwa kupakua Aplikesheni (APP) ya eTS hatua itakayomwezesha mfanyabiasha kutambua uhalali wa bidhaa zake ili kuweza kulinda ya fya ya mtumiaji.
Kwa upande wake Afisa Elimu kwa Mlipa kodi na Mawasiliano wa TRA Mkoa wa Kilimanjaro, Oldupai Papaa amesema katika kipindi hiki za Sikuku za mwisho wa mwaka zoezi la ukaguzi wa bidhaa litaimarishwa maradufu.
Baadhi ya wafanyabiashara nao wamepongeza zoezi hilo na kwamba litawawzesha kutambua bidhaa bandia.