28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Halotel yafanya usafi soko la Makumbusho

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Halotel pamoja na wafanyakazi wake wemeshiriki katika zoezi la usafi soko la Makumbusho jijiji Dar es Salaam katika kusherehekea Sikukuu za mwisho wa mwaka. 

Aidha, mazingira safi na salama huchochea katika ufanisi katika shughuli mbalimbali za kujitafutia kipato ambapo Halotel kwa kushirikiana na Ofisi ya Diwani kata ya Kijitonyama imeshiriki zoezi hilo kwa kusafisha soko la Makumbusho katika jitihada za kuweka mazingira safi.

Wakati huo huo tukio hilo lilihudhuriwa na kuungwa mkono na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ambapo ameonyesha kufurahishwa na kitendo kilichofanywa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na kata ya Kijitonyama pamoja na viongozi wengine huku swala hili likiwa ni kuunga mkono sekta ya ustawi wa jamii kwa maslahi ya taifa.

“Gharama ya uchafu ni kubwa na utatuzi wake ni mgumu hivyo kila mwananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam achukulie kwa ukubwa, usafi ni mhimu kwa ustawi wa jamii yoyote hapa nchini,” amesema Chalamila. 

Aidha, ametoa maagizo kwa watendaji wake kuhakikisha kila Jumamosi ya mwisho wa munafanyika usafi ili kupunguza kasi ya maradhi yanayotokana na uchafu.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Sekta ya Biashara ya Kampuni ya Halotel, Abdallah Salum, amesema katika kuhakikisha haraka za upambanaji ni muhimu kushiriki katika jamii kwa maswala ya usafi ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa mbalimbali vya usafi ili mazingira ya biashara yawe safi.

“Tunatambua changamoto zinazoikumba sehememu yenye mchanganyiko wa  wafanyabiashara wengi kama hapa sokoni, hivyo kukiwa na vifaa kama reki, fagio na dustbin itapunguza kuzagaa kwa taka katika soko hili,” alisema Salum.

Kwa upande wa mfanyabiashara, Fatuma Musa, amesema kuwa ni furaha kuona kampuni kama Halotel kutambua thamani ya wafanyabiashara kisha kushiriki katika swala la usafi na kuleta vifaa mbalimbali vitakavyorahisha kuweka mazingira safi ya soko hilo.

Amesema Halotel itaendelea kupiga hatua kubwa katika kusambaza huduma za Mawasiliano na kutoa huduma zenye ubora nchi nzima, kampuni hii itaendelea kujihusisha na kutoa misaada mbalimbali kwa jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles