31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

TPDC yawatoa hofu Watanzania kuhusu usalama gesi asilia

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limewatoa hofu Watanzania kuhusu usalama wa gesi asilia kwa kueleza kuwa nishati hiyo ni salama na haina athari hata pale inapotokea imevuja.

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani, akikagua migahawa iliyounganishiwa gesi asilia iliyopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na baadhi ya nyumba zilizounganishiwa nishati hiyo katika eneo la Mwenge Mlalakuwa hivi karibuni (Picha na Maktaba).

Hayo yameelezwa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dk. James Mataragio, ambapo amesema kuwa gesi asilia ni tofauti na ile inayotumika kwenye mitundi ya kawaida kwa kuwa ni nyepesi.

“Niwaondoe tu hofu Watanzania kuhusu usalama wa gesi asilia kwani gesi hii ni salama zaidi ikilinganishwa na aina nyingine ya nishati kama ilivyo zile ya mitungi, mkaa au kuni.

“Gesi asilia ni nyepesi sana kwa hivyo inapotokea ikavuja inayeyuka na kupotea hewani haraka sana na hata utakapowasha kiberiti hakuna athari yoyote itakayotokea, jambo la msingi ni kwa watumiaji kufuata maelekezo ya usalama ambayo yatakuwa yanatolewa na wataalamu wetu mara kwa mara,” amesema Dk. Mataragio.

Akizungumzia unafuu wa matumizi ya gesi asilia Dk. Mataragio amesema kuwa nishati hiyo makadirio ya matumizi kwa familia ya watu sita ni wastani wa Sh 29,000 kwa mwezi sawa na Sh 1,000 kwa siku hii ikihusisha kupika vyakula vinavyochukua muda mrefu.

“Gharama hizi zimekadiriwa kutoka kwenye takwimu za watu wengi ambao wameanza kutumia gesi asilia tangu mwaka 2005,” amesema Dk. Mataragio na kuongeza kuwa nishati hiyo inaenda kubadilisha maisha ya wananchi

Aidha, Dk, Mataragio amebainisha kuwa miradi mingi ya gesi asilia kwa sasa inatekelezwa na Watanzania hatua ambayo inaongeza mafanikio makubwa kwenye sekta hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles