25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yakabidhi msaada wa mabati 950 ujenzi wa madarasa Babati

Na Mwandishi Wetu, Babati

Benki ya NMB nchini imetoa msaada wa mabati 950 kwa ajili ya shule sita za sekondari zilizopo wilayani Babati ikiwa ni kuunga mkono  juhudi za Serikali katika ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwawiki katika shule ya seondari Galapo Wilayani Babati  na mgeni rasmi katika makabidhinao hayo  alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara ,Joseph Mkirikiti  

Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Joseph Mkirikiti, (kushoto) akipokea msaada wa mabati  kutoka  kwa Meneja wa Nmb Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi (wapili kulia) katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika mwishoni mwa juma katika shule ya Sekondari Galapo wilayani Babati mkoani Manyara.Wengine katika picha ni Meneja Mahusiano  ya Serikali wa NMB kanda ya kati – Peter  Masawe (wa pili kulia na  meneja wa Nmb Tawi la Babati ,Antiphas Nnko (kulia).

Akizungumza wakati wa kukabidhino  hayo,  meneja wa NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi, amesema msaada huo wa NMB ni kuunga mkono juhudi za Serikali kuhusu ujenzi wa vyumba vya madarasa.

“Msaada huu tuliokabidhi leo ni  kuunga mkono juhudi za serikali yetu katika kuhakikisha kuwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu wanaingia madarasani bila kukosa,” amesema.

Mlozi alitaja thamani ya mabati hayo yaliyotolewa kuwa ni zaidi ya sh milioni 28.1 kwa jili ya shule sita za sekondari zilizopo wilayani hapa.

Shule zilizofaidika na msaada huo ni pamoja na shule za sekondari  Magugu,Galapo,Madunga, Nar, Qash na Aytesea.

Aidha amesema Nmb imekuwa ikitoa misaada kwenye Jamii huku lengo kuu likiwa ni kurudisha fadhila kwa jamii kutokana na faida  inayoipata kila mwaka kwasababu ya wananchi kuunga mkono benki katika  kutumia  huduma za kifedha wanazotoa

Kadhalika ameongeza kuwa misaada hiyo imekuwa ikielekezwa kwenye maeneo muhimu ya kutolea huduma za kijamii hasa sekta ya afya,elimu na wakati wa majanga .

Naye Mkurungenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Babati Vijijini, John Nchimbi, amewashukuru NMB kwa msaada waliotoa huku akisisitiza kuwa benki hiyo imekuwa ni mkombozi kwa wananchi wanyonge kutokana na kutoa misaada hiyo

Nchimbi amesema   msaada uliotolewa umewapunguzia mzigo wazazi kwani wagetakiwa kuchangia ujenzi huo wa madarasa ambao unagharimu fedha nyingi.

Mkurungenzi huyo alisema baada ya msaada huo wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza  503 ambao walioshindwa kujiunga  na masomo atakuwa na uhakika wa kuingia darasani wiki ijayo na walikuwa na upungufu wa vyumba 13 katika Halamshauri hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti amezitaka kamati za shule kuhakikisha wanatafuta mafundi bora wa kupaua mapaa ya mabati ili kuepuka kuharibu mabati wakati wa ujenzi.

Mkirikiti amesema NMB wameipunguzia serikali mzigo kwa kusaidia mabati kwaajili ya kupaua na hivyo kusaidia wanafunzi wengi watakaosoka katika shule hizo kwa vizazi vijavyo kwani shule zinakaa na kuhudumia watu wengi zaidi.

Hata hivyo amesema katika Halmshauri zake saba za Mkoa huo alikuwa na mzigo mkubwa kwa halmashauri ya Babati Vijini lakini kwa sasa anashukuru kupunguziwa mzigo huo na benki ya NMB.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles