25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Muleba waomba kuanza kutumika kwa majengo yaliyokabidhiwa kwa ajili ya kituo cha Afya

Na Mwandishi Wetu, Kagera

Wananchi Kata ya Ijumbi wilayani Muleba mkoani Kagera wameomba majengo matatu yaliyokabidhiwa kwa Halmashauri kwa ajili ya matumizi ya Kituo cha Afya yaanze kutumika ili waweze kupata huduma ya matibabu kwenye kata hiyo.

Wananchi hao walizungumzia majengo hayo jana wakati wakieleza changamoto wanazokabiliana nazo wanapohitaji matibabu.

Akizungumza kwaniaba ya wanakijiji wenzake, Petruinda Rwiza, amesema uwepo wa kituo hicho utawaondolea changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya katika hospitali teule ya wilaya Rubya.

“Si hivyo tu bali itatusaidia kupata huduma za dharula hasa pale mtu anaposhikwa ugonjwa ghafla nyakati za usiku,” amesema Petruinda.

Diwani wa Kata Ijumbi, Wilbad Kakuru. akionyesha majengo yaliojengwa na mdau wa maendeleo, Prosper Rweyendera, na kuyakabidhi kwa Serikali ya Kijiji hicho kwa muda mrefu bila kufanyiwa kazi ikiwemo huduma ya afya.

Akizungumzia hilo Diwani wa Kata ya Ijumbi, Wilbard Musirigi, amesema majengo matatu yalitolewa na Mfadhili, Prosper Rweyendera, mwaka 2019 kwa ajili ya Kituo cha Afya lakini yakihitaji ukarabati wa miundombinu ili kuyaweka katika mfumo wa Kituo cha Afya.

“Katika bajeti ya mwaka 2020/2021 Serikali ilitenga Sh milioni 50 kwa ajili ya kukarabati majengo mawili, kujenga kichomea taka, nyumba ya Mganga na Theatre.

“Kwa mwaka huu ukarabati utafanyika pamoja na kukisajili Kituo, mahitaji ya huduma ya afya ni makubwa kwani kati ya Kata sita zinazokizunguka Kijiji cha Rubao ni kata moja tu yenye Zahanati, kata zote zinategemea huduma kutoka kwenye Kituo hicho kikianza kutoa huduma,” amesema Musirigi.

Afisa Mtendaji wa Kata hiyo, Salehe Mruma alisema kwa sasa majengo hayo yanatumika kwa ajili ya Kliniki ya Mama na Mtoto. 

Amesema vijiji viwili vinapata huduma hiyo Ijumbi na wananchi wengine kutoka maeneo mengine kila mwezi na watumishi wa kutoa huduma wanafika kituoni hapo kwa ratiba.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ijumbi iliyopo Muleba mkoani Kagera, Saleh Mruma kulia, akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu kutaka kuanza kuyafanyia marekebisho majengo yaliojengwa na mdau wa maendeleo kijijini hapo, Prosper Rweyendera, baada ya kuwakabidhi kwa matumizi ya mbalimbali ikiwemo huduma za Afya, kushoto ni Diwani wa Kata hiyo, Wilbad Kakuru.

Aidha, Mruma ameomba aliyewafadhili majengo hayo asichoke kufanya hivyo kwani mahitaji bado ni mengi.

“Baadhi ya miundombinu inaweza kuchelewa, anaweza kutusaidia hayo mahitaji ili kukamilisha haraka ukarabati,” amesema Mruma.

Mruma amesema alisaini mkataba wa kukabidhiwa majengo hayo pamoja na Diwani Musirigi mwaka 2019.

Amesema makabidhiano yalikuwa kati ya, Prosper Rweyendera, ambaye ni mmiliki wa majengo na Halmashauri ya Muleba pamoja na Halmashauri ya Kijiji cha Rubao.

Majengo hayo yenye thamani ya Sh 149,442,531 yalikabidhiwa bure kwa makubaliano kwamba yaanze kutumika kutoa huduma za afya ndani ya miaka mitatu.

Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk. Modest Rwakehemura, akizungumzia Kituo hicho cha afya amesema ukarabati wa majengo utaanza hivi karibuni na Huduma rasmi zitaanza mwaka ujao wa fedha (2021/22).

Amesema kwa kuanzia, kutuo kitatoa huduma za upasuaji wa dharula kwa mama wajawazito na zingine zote zinazohusu mama na mtoto.

“Tunazingatia pia mahitaji ya Theater na leba (labour) kwa Huduma zaidi za upasuaji, tutakua tukiimarisha Huduma kwa awamu kulingana na bajeti inavyoruhusu.

“Pia tunashukuru kwamba wadau wengine wanajitokeza kuunga mkono juhudi za mfadhili wa kwanza aliyetupatia majengo haya matatu,”amesema Dk.Rwekehemura. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles