25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Daraja la Magufuli ziwa Victoria lafikia asilimi 17

Na Sheila Katikula, Mwanza

Mradi wa ujenzi wa daraja la Magufuli  lililopo jijini Mwanza ulianza kutekelezwa Februari Mwaka 2020 na Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation na China Railway 15 Group Corporation pamoja na ujenzi  wa barabara unganishi zenye urefu  wa kilometa 1.66 umefikia asilimia  17.3.

Hayo aliyasema jana  na  Kaimu Meneja wa Wakala  wa  Barabara (TANROADS), Mhandisi Vedastus Maribe, wakati akizungumza na MtanzaniaDigital ofisini kwake ambapo amesema mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka minne na utaghalimu Sh bilioni 700.

Amesema mashimo ya msingi yanaendelea kuchimbwa  kwani hivi sasa  daraja hilo limefikia asilimia 17.3 na ujenzi unaendelea  kwani lengo ni kuhakikisha mradi huo unamalizika kwa wakati.

Abainisha kuwa daraja hilo hadi hivi sasa limeshajengwa urefu  wa mita 1558   kigongoferi na busisi  mita 444 jumla  ya mita 2002   kati ya 3200 na kufikia asilimia 62.5 kwenye daraja la muda.

Ameongeza kuwa mradi huo umewapa kipaumbele wazawa kwa kuwapatia nafasi za ajira ili kuwainua kiuchumia.

“Mradi huu wa ujenzi wa daraja umetoa ajira kwa vijana  wengi kutoka sehemu mbalimbali  na kupelekea kutatua changamoto ya ajira,” amesema Maribe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles