29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Gwiji wa kusafirisha wahamiaji haramu anaswa Mwanza

Na Sheila Katikula, Mwanza

Kinara wa usafirishaji wa wahamiaji haramu, David Kapangala (31) na wenzake watatu wamekamatwa mkoani Mwanza na Idara ya Uhamiaji  kwa kosa la kuwahifadhi na kuwasafirisha wahamiaji haramu kutoka nchi mbalimbali.

Akizungumza na Waandishi wa Habari  ofisini kwake  Kamishina  wa Idara ya  Uhamija Mkoa wa Mwanza, Bahati Mwaifuge, amesema wanawashikilia watuhumiwa hao kwa kosa la kuwahifadhi, kuwasafirisha  wahamiaji haramu 54 wakiwamo Warundi 13 ambao ni wanawake, Mkenya mmoja na  Waethiopia 11 na watanzania wanne ambao wamekamatwa kwa nyakati tofauti.

Amesema idara hiyo imewatia nguvuni wahusika warioshiriki kuwahifadhi kwenye  nyumbani hiyo iliyopo mtaa wa Majengo Mapya Kata ya Mkolani  kwa kuwatunza wahamiaji hao.

“Tulikuwa tukimtafuta tangu siku nyingi David, tulienda hapo alipopanga kwa lengo la kumkamata  tulipofika  baada ya kufanya ukaguzi tukagundua kuna watu juu ya dari tulipowaambia washuke  walitoka watu 11,” amesema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, amewataka wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya kutunza na kusafirisha wahamiaji hao  kwani kufanya hivyo ni kosa na sheria zitachukuliwa ili iwe fundisho  kwa wengine.

Hata hivyo amelipongeza jeshi hilo kwa jitihada zao za  kufanya kazi usiku na mchana  na  kupelekea kuwakamata wahamiaji hao jijini hapa.
“Nawaomba wananchi wajishughulishe na kazi za kilimo kwani mvua zinaendelea kunyesha   waache kufanya kazi  ambazo siyo za halali,” amesema Mongela.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Mapya iliyopo Kata ya  Mkolani,  Ramadhan Musabi, amewataka wananchi kutoa taarifa  kwa jeshi la polisi ili kuepusha  vitendo hivyo,kwani mtuhumiwa huyo  mara ya kwanza waliwakamata wahamiaji  kwenye eneo la nyumba ya David wakiwa kwenye gari likiwa limepaki kwenye shama la mahindi.

“Viongozi wa mitaa washirikiane na wananchi ili waendelee kubaini vitendo vya uharifu na wasikubali kudanganyika na rushwa ndogo ndogo bali waendeleze uzalendo wa nchi,”amesema Musabi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles