26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

TOC wamuomba Waziri Bashungwa kukutana nao

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

KAMATI ya Olimpiki Tanzania (TOC) imemwomba Waziri mpya  wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa kukutana nao ili wampe ushauri wanatakiwa kufanyaje ili kuendeleza michezo nchini.

Jana Rais Magufuli wakati akiwaapisha Mawaziri na Manaibu Mawaziri Ikulu Chamwino jijini Dodoma alimtaka Waziri Bashungwa na Naibu wake,Abdallah Ulega kuhakikisha wanaendeleza michezo nchini na kuja

Akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa Kamisheni ya Wanaompiki Tanzania (TOA), leo Desemba 10 mwaka huu jijini Dodoma, Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau amesema  Rais Magufuli ni mdau wa michezo na anataka kuona sekta hiyo inakuwa ndio maana alitoa maagizo kwa Mawaziri wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kuhakikisha wanasaidia kuendeleza michezo.

Amesema wao kama wadau wa michezo wapo tayari kutoa ushauri wao ili kuhakikisha michezo inaendelea kutoa ajira pamoja na nini kifanyike ili kuendeleza sekta hiyo.

“Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alimwapisha Waziri(Innocent Bashungwa  na Naibu Waziri (Abdallah Ulega) wenye dhamana ya michezo na aliwataka wahakikishe tunafanya vizuri naamini kama wanamichezo tutakuwa na mchango wa nini kifanyike ili wanamichezo tuweze kufanya vizuri.

“Ni vizuri tujitayarishe tutakapotakiwa kutoa maoni yetu tuwe vizuri sio tunaitwa tunasema subiri ni imani yangu mtakayozungumza tuangalie maeneo mazuri ya kuwasilisha,”amesema.

Hata hivyo, Tandau amesema tayari wameishapeleka mpango wa Taifa wa michezo Oktoba mwaka huu kwa Wizara ya Habari,Utamaduni na Sanaa kuhusiana na mambo mbalimbali ikiwemo marekebisho ya sheria ya michezo ambayo haina msaada kwa mwanamichezo.   

“Kwa muda mrefu tumekuwa hatuna mpango  wa Taifa wa michezo na  Mkakati upo tayari na umekabidhiwa kwa Rais kupitia kwa Waziri mwenye dhamana mwezi Oktoba sasa mategemeo yetu ni kupitiwa na kutekelezwa.

“Mpango huo una mambo kama saba ambayo ni pamoja marekebisho ya sheria ya michezo  sio rafiki  kwa michezo katika mazingira ya leo.Nafikiri itafika wakati wa kupokea maoni juu ya marekebisho hayo niombe wakati huo utakapofika tujitokeze tutuoe ushauri,”amesema.

Tandau amesema eneo lingine ambalo linatakiwa kuangaliwa katika mpango huo ni pamoja na kuboresha maslahi ya wanamichezo pindi wanapostaafu.

“Tumefanya hivi kwa kuzingatia wanamichezo wengi baada ya kustaafu maisha yao  yanakuwa sio mazuri ni muhimu tutengeneze utaratibu mzuri wa kuidi jasho lao,”amesema.

Kwa upande wake,Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi amesema wanatarajia kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa Kamisheni ya wanaolimpiki Tanzania ambapo alidai sifa za wagombea ni lazima wawe wameshiriki Mashindano ya Olimpiki kwa vipindi vitatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles