24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

TMA wapimeni watendaji wavivu – Prof. Mbarawa  

Prof. Makame MbarawaKOKU DAVID NA MAULI MUYENJWA, DARE S SALAAM.

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, ameitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kuwa na utaratibu wa kupima utendaji wa watumishi wake ili kubaini watendaji wavivu waondolewe kazini.

Waziri Mbarawa alitoa kauli hiyo juzi, alipotembelea ofisi za TMA zilizopo jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam kwa lengo la kufahamiana na kupeana mikakati ya kazi.

Aliwataka watendaji kwenda na kasi ya Serikali ya awamu ya tano, ambayo imedhamiria kuondoa kero za wananchi.

Prof. Mbarawa alisema ili kufanikisha malengo ya TMA ya kuchochea maendeleo katika jamii kwa kutoa taarifa za hali ya hewa za uhakika, lazima wafanyakazi wawe na uadilifu, uwazi na ubunifu.

Alisema wafanyakazi wote wanatakiwa kufanya kazi kwa ukaribu na kuthaminiana kuanzia ngazi ya juu hadi chini ili kupeana taarifa kwa urahisi.

“Kuanzia mwaka huu, tutapeana mikataba ya kazi, mimi nitaingia mkataba na mkurugenzi wa bodi kwa kupeana mikakati ya kazi na baada ya muda nitakuja kuikagua, kama atakuwa hajaitekeleza, basi mlango alioingilia ndiyo atakaotokea.

“Mkurugenzi mkuu ataingia mkataba na Katibu Mkuu wa Wizara na yeye ataingia mkataba na wakurugenzi wake ambao nao wataingia mkataba na watendaji wao ili atakayeshindwa kwenda na kasi hii aondoke kwa kutumia mlango alioingilia,” alisema Prof. Mbarawa.

Aliwataka kutumia fursa za utunzaji wa takwimu kwa kutumia kituo kipya cha kutunzia takwimu kilichopo Mwananyamala.

Alisema wanatakiwa kuacha kuandika madokezo kwa kutumia karatasi kutokana na kuwa wanaiingizia Serikali gharama ambazo hazina sababu za msingi na badala yake wanatakiwa kwenda na wakati kwa kutumia mitandao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles