30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Watelekeza misokoto ya bangi 4,500

Wilbrod MutafungwaNa Upendo Mosha, Siha

WATU wawili wanaodhaniwa kuwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, wamewakimbia polisi na kutelekeza kilo 10 za bangi na misokoto 4,500 iliyokuwa ikisafirishwa kwa pikipiki.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod Mutafungwa, alikiri kukamatwa kwa bangi hiyo na watuhumiwa kutoweka.

Kamanda Mutafungwa alisema watuhumiwa waliwakimbia askari, Aprili  15, mwaka huu saa 8:30 mchana wilayani Siha.

Alisema polisi wakiwa doria eneo la Mwisho wa Lami, Sanya juu, walikamata bangi hiyo ambayo ilikuwa inasafirishwa kwa kutumia pikipiki aina ya Toyo yenye namba za usajili MC 610 ATT.

Kamanda Mutafungwa alisema katika tukio hilo, watuhumiwa wawili walikimbia baada ya kuwaona askari na kutelekeza pikipiki hiyo pamoja na bangi kilo 10, misokoto ya bangi 4,500 sawa na kilo gramu 13.5.

“Polisi walikimbiwa na watuhumiwa wawili ambao walikuwa wakisafirisha bangi, walitokomea kusikojulikana na kutelekeza pikipiki waliyokuwa wakitumia,” alisema Kamanda Mutafungwa.

Alisema hadi sasa polisi bado inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

“Tunatoa onyo kwa wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro ambao wanajihusisha na vitendo vya uhalifu, vikiwamo uporaji, kujihusisha na biashara na matumizi ya dawa za kulevya kuacha mara moja, tumejipanga vizuri,” alisema Kamanda Mutafungwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles