31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge: Pinda alitaka kuchomokea dirishani

pinda5NA ELIZABETH HOMBO, DODOMA

MBUNGE wa Ulanga, Gudluck Mlinga (CCM), amesema Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, alitaka kuchomokea dirishani baada ya kutoswa katika uteuzi wa urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Mlinga ambaye pia ni mtoto wa marehemu, Selina Kombani, alitoa kauli hiyo juzi jioni, wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Alisema baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuhamia upinzani na wenzake, Pinda naye alitaka kuwafuata, lakini akashtuka na kubaki CCM.

“Yule mwingine alituzingua tukampiga chini akaenda upinzani, Pinda naye mwaka jana alitetereka, tukamtosa akataka kuchomokea dirishani… akashtukia akabaki, kwahiyo CCM hatufanyi mambo kwa kuambiwa kama wanavyofanya upinzani,” alisema.

Kauli ya Mlinga ilionekana kumkera Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy (CCM) ambaye aliomba kutoa taarifa: “Mheshimiwa mwenyekiti nampa taarifa mzungumzaji, amemvunjia heshima Pinda kwa kusema alitokea dirishani, afute kauli yake mara moja au athibitishe ni lini Pinda alitokea dirishani… mtoto huna adabu, huna nidhamu,” alisema Keissy huku akishangiliwa na wabunge wa upinzani.

Baada ya taarifa ya Keissy, mwenyekiti akamtaka Mlinda kuendelea kuchangia na kujikita kwenye hoja.

“Pamoja na umbile langu ndogo, leo nipo hapa kuwapa semina wabunge wa upinzani. Huyo mwenyekiti wenu namfahamu kwa sababu nimeoa huko, kwahiyo aibu yake aibu yangu, na hata ile hotuba yake aliandikiwa hapo mlangoni… mimi ningekuwepo asingetoa.

“Wabunge wa upinzani waelewe nimewaambia  natoa somo kwao na naomba nitoe mfano mwingine. Haya mambo ya mnakaa hapa eti mwenyekiti kasema, kila kitu mwenyekiti… mimi namfahamu huyo mwenyekiti wenu kwa sababu nimeoa huko, tangu nampata binti yao yeye ni mwenyekiti, nimeoa yeye ni mwenyekiti hadi nimezaa mtoto wa pili bado yeye ni mwenyekiti.

“Juzi nilisikitika sana kuna mmoja alikuwa anahoji mshahara wa Rais, yeye anachangia chama Sh milioni tatu kila mwezi… sasa hizo fedha zinakwenda wapi?” alihoji ,” alisema Mlinga ambaye alitumia muda wake wote kuvishambulia vyama vya upinzani, huku akizomewa na wabunge wa upinzani wakimwambia “teja huyooo”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles