28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 21, 2024

Contact us: [email protected]

TLS kushirikiana na Serikali utoaji msaada wa kisheria kwa Wananchi

Na Mwandisi Wetu, Mtanzania Digital

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali na wadau wa sekta ya sheria katika kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi.

Kauli ya Mwabukusi aliyoitoa Oktoba 19, 2024 inathibitisha jukumu kubwa la serikali katika kuhakikisha haki inafikiwa na raia wote, hususan wale walioko kwenye mazingira magumu.

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imejitolea kwa dhati kusaidia makundi haya kwa kushirikiana na mashirika kama TLS. Kupitia ushirikiano huo, serikali inahakikisha huduma za msaada wa kisheria zinapatikana kwa urahisi, huku zikizingatia kanuni za haki za binadamu na utawala wa sheria.

Mwabukusi alibainisha kuwa wito wake wa kushirikiana na serikali unalingana na ajenda ya serikali ya Rais Samia ya kuimarisha haki na demokrasia. Serikali imekuwa ikisisitiza mara kwa mara umuhimu wa kujenga taasisi imara zinazolinda haki za binadamu na kutoa huduma bora kwa umma. Serikali inafanya kazi kwa mujibu wa wajibu wake wa kuhudumia raia wote, bila kujali hali zao za kifedha, na wala haiendeshwi na misukumo ya kibinafsi au hisia.

TLS, kwa upande wake, inaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kukuza haki za binadamu na kuimarisha utawala wa sheria. Katika juhudi hizi, jukumu la serikali linabaki kuwa muhimu katika kutoa rasilimali na kuunda mazingira bora kwa ajili ya kufanikisha malengo haya.

Kwa pamoja, ushirikiano kati ya TLS na serikali utahakikisha kuwa wananchi wa Tanzania wanapata msaada wa kisheria wanaostahili, hatua ambayo itaimarisha zaidi demokrasia ya nchi na mfumo wa haki.

Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan unaonesha dhamira thabiti ya kuhakikisha ustawi wa wananchi na maendeleo ya haki za binadamu. Kwa kushirikiana na TLS, serikali inachukua hatua kubwa katika kujenga jamii jumuishi na yenye haki, huku ikidumisha utawala wa sheria kwa vitendo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles