28.4 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

TIGO YAZINDUA TWENDE APP KUSAIDIA USAFIRI WA TEKSI

 

Taxi

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya simu ya Tigo imezindua huduma mpya ya kidigitali inayoitwa Twende App ambayo ni suluhisho la kuita teksi na kuwapatia wateja wake huduma sahihi na wanayoimudu nchini.

Kwa kuunganishwa moja kwa moja na madereva wa teksi, huduma hiyo inawawezesha watumiaji kufurahia kiwango cha chini kuliko ambavyo wangetumia njia nyingine mbadala za mitaani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Huduma za Kidijitali wa Tigo, Tawonga Mpore, alisema huduma hiyo ni kielelezo cha Tigo kujikita katika mageuzi ya mtindo wa maisha ya kidijitali kwa kutoa suluhisho kwa changamoto zinazowakabili wateja wake.

“Tunaamini kuwa Twende App itatoa huduma nzuri kwa abiria kwa kuwaunganisha  na madereva ambapo watapata huduma bora na za gharama nafuu,” alisema.

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Hassan Mshinda ambaye aliishukuru Tigo kwa kubuni mbinu nzuri zitakazowasaidia vijana kumudu maisha na kwamba amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wajasiriamali vijana wanapata msaada muhimu katika teknolojia ya kisasa.

Alisema katika kufikisha malengo yao na kwa huduma hiyo, anaamini itawapatia fursa mpya zenye manufaa kwa madereva wote jijini Dar es Salaam.

Naye Ofisa Mtendaji na Mwasisi wa Twende App, Justin Kashaigili, alisema amesukumwa na kasi ya maendeleo ya mbinu na nguvu ya ujasiriamali nchini.

“Ninatarajia kuwapatia wakazi wa Dar es Salaam chaguo wanalolimudu, rahisi na linalofaa kwa ajili ya usafiri salama,” alisema.

Alisema ili kujiunga na huduma hiyo, abiria anatakiwa kupakua Twende App katika simu yake ambayo itamuunganisha na dereva moja kwa moja badala ya kuhangaika kwenda mwenyewe kufuata sehemu ilipo teksi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles