YAHYA JAMMEH AGOMA KUACHIA NGAZI GAMBIA

0
610
Rais Jammeh Gambia
Rais wa Gambia Yahya Jammeh

Rais wa Gambia Yahya Jammeh amekataa kuondoka madarakani kutoa nafasi ya kuapishwa kwa Adama Barrow hata baada ya ‘deadline’ aliyopewa na Senegal kumalizika.

Barrow alipangiwa kuapishwa kuwa rais mpya Alhamisi, na hii ni baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu mwezi uliopita.

Katika hili, Rais Jammeh mwanzoni alikubali kushindwa lakini baadaye akapinga matokeo hayo.

Pamaoja na mambo mengine, pendekezo la wanajeshi wa mataifa ya Afrika Magharibi kuingilia kati kumuondoa madarakani Jammeh linaungwa mkono na Nigeria na nchi nyingine za kanda hiyo.

Jammeh ametawala Gambia tangu alipochukua madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1994.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here