The Game amsaka aliyevunja gari lake

0
726

The GameLOS ANGELES, Marekani

MSANII wa hip hop nchini Marekani, Jayceon Taylor ‘The Game’, amesema anamtafuta mtu aliyevunja vioo vya gari lake aina ya Lamborghini.

Mtandao wa TMZ umeeleza kwamba, msanii huyo alivamiwa na watu wasiojulikana na kuvunja vioo vya gari hilo likiwa limeegeshwa eneo la barabara.

Kupitia akaunti ya mtandao wa Instagram, msanii huyo amesema anamtafuta mtu aliyehusika na tukio hilo ili akabiliane naye.

“Kama kuna mtu anamjua mhusika wa tukio hilo anijulishe, nitatoa zawadi nono, ninaamini atapatika,” alisema The Game kwa hasira.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here