NYOTA wa mbio za magari, Lewis Hamilton, amepigwa marufuku na mchumba wake, Nicole Scherzinger, kuendelea kuwasiliana na mwanamitindo na mwanamuziki mashuhuri nchini Marekani, Rihanna.
Kauli ya mwanadada huyo kumpiga ‘stop’ mpenzi wake huyo kunatokana na tetesi kwamba nyota huyo wa mbio za magari ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Rihanna.
“Nimemwambia Hamilton akate mawasiliano na Rihanna na kama hataki akate mawasiliano na mimi ili wawe na uhuru.
“Nimempa muda wa kukata mawasiliano na Rihanna, ikishindikana nitajua cha kufanya, sitaki kugombana na mtu ila nataka wawe waelewa,” alisema Nicole.
Rihanna baada ya kuachana na mkali wa RnB, Chris Brown, amekuwa akitajwa kutoka na wanaume mbalimbali akiwemo mchezaji wa timu ya Ligi Kuu ya Hispania, Real Madrid, Karim Benzema na wengine wengi.