23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

TFF yajitoa kuandaa Kagame

Alfred-LucasNA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

SHIRIKISHO la soka Tanzania ‘TFF’ limejitoa kuandaa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ‘Kagame’ kwa madai ya kubanwa na ratiba ya michezo mbalimbali ya kimataifa kati ya Juni na Septemba mwaka huu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Baraza la vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), kutaka michuano hiyo iliyotarajiwa kuanza Juni 16 hadi Julai 2 mwaka huu, kuchezwa jijini Dar es Salaam kwa mara ya pili badala ya Zanazibar ilikopangwa awali.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema shirikisho hilo halitaandaa mashindano hayo kutokana na mwingiliano wa ratiba ya kimataifa.

“Cecafa walitaka michuano hii ifanyike Juni 16 mwaka huu, yaani muda mchache baada ya kumaliza mchezo wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2017), unaotarajiwa kuchezwa Juni 4 dhidi ya Misri.

“Wakati huo wachezaji wa timu ya Taifa hasa wa Yanga watakuwa wakijiandaa na mchezo wa nane bora, unaotarajiwa kuchezwa Juni 17 nchini Algeria,” alisema Lucas.

Alieleza, TFF pia inakabiliwa na maandalizi ya timu ya vijana Juni 25 mwaka huu, kwa ajili ya mchezo dhidi ya Shelisheli wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 yatakayofanyika mwakani nchini Madagascar.

Katika mashindano ya mwaka jana ya Kombe la Kagame, timu ya Azam FC waliibuka mabingwa baada ya kuifunga Gor Mahia ya Kenya.

Wakati huo huo Lucas alisema kuwa timu ya Taifa ‘Taifa Stas’, itaondoka leo kuelekea Kenya kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu kabla ya mchezo wao dhidi ya Misri.

“Kesho (leo) timu ya taifa itaelekea Kenya kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kimataifa, ambao matokeo ya ushindi ni muhimu ili kuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kusonga mbele,” alisema Lucas.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles