29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

TFF YADAI POINTI ZA SERENGETI BOYS CAF

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM


afisa-habari-wa-tff-alfred-lucas

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeandika barua kwa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kudai pointi tatu za mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Congo Brazzaville.

TFF inadai pointi hizo baada ya Congo kumchezesha mchezaji Langa Lesse Bercy anayedaiwa kuzidi umri katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, kilichovaana na Serengeti Boys.

Katika mchezo wa marudiano, Congo ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Bercy na kufanikiwa kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana zitakazofanyika mwakani nchini Madagascar, baada ya awali kufungwa mabao 3-2 ugenini.

Mchezaji huyo alitakiwa kuwasili nchini Misri Novemba 19, mwaka huu ili kufanyiwa vipimo vya uchunguzi kuhusu umri wake, lakini inadaiwa alishindwa kufika kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema barua ya kudai pointi tatu ilitumwa juzi, baada ya kugundua makosa ya wapinzani wao ya kumchezesha mchezaji huyo aliyezidi umri unaotakiwa na CAF.

Alisema TFF inatarajia kujibiwa barua hiyo ndani ya siku mbili, ambapo kama  CAF itaridhia na kuinyang’anya pointi Congo, Serengeti Boys itakata tiketi ya kucheza fainali za mwakani.

“Tunafuatilia jambo hili kwa umakini wa hali ya juu maana kuna kila dalili ya wapinzani wetu kupokonywa pointi, hivyo tunasubiri majibu ya CAF baada ya siku mbili,” alisema Lucas.

Kwa mujibu wa kanuni za CAF, udanganyifu wa umri ni kosa ambalo linaweza kupelekea nchi husika kufungiwa kushiriki mashindano husika kwa muda wa miaka mitatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles