24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MKUTANO WA DHARURA SIMBA DESEMBA 11

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM


simba-vs-yanga-2

KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Simba chini ya Rais Evance Aveva, imeitisha mkutano wa dharura unaotarajiwa kufanyika Desemba 11, mwaka huu katika ukumbi wa bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay kwa ajili ya kujadili mabadiliko ya katiba.

Awali Baraza la Michezo Taifa (BMT), kupitia katibu wake, Mohamed Kiganja, lilisitisha michakato yote inayoendelea ndani ya klabu ya Simba na Yanga, kubadili umiliki wa timu kutoka kwa wanachama kuelekea kwenye umiliki wa hisa na ukodishwaji, hadi hapo watakapofanya marekebisho ya katiba zao.

Wakati BMT inatoa kauli hiyo, Simba ilikuwa katika hatua ya mwisho ya kumkabidhi klabu hiyo mfanyabiashara, Mohammed Dewji ‘Mo’ kwa umiliki wa hisa za asilimia 51.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara, alisema mkutano huo ni mwendelezo wa maazimio ya mkutano mkuu wa kawaida uliofanyika Julai 31, mwaka huu ambao kwa kauli moja uliazimia kubadili mfumo wa uendeshaji wa klabu.

“Nyaraka zote muhimu zitakabidhiwa kwa wanachama kupitia matawi yao kwa mujibu wa matakwa ya katiba, ibara ya 22 kifungu cha nne na Katiba ya klabu,” alisema.

Alisema kamati hiyo iliyokutana Novemba 11, mwaka huu jijini hapa, imetumia mamlaka iliyopewa na Katiba ya Simba, ibara ya 22 kifungu cha kwanza.

Hivi karibuni kamati hiyo ilikutana Agosti 15, mwaka huu na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa makampuni ya Mohammed Enterprises Limited (MeTL), Mohammed Dewji, ambaye aliomba kununua asilimia 51 ya hisa za Simba kama mfumo ukibadilika na kuanza kuendeshwa klabu hiyo kwa hisa, ambapo Agosti 17, mwaka huu Simba walitoa  makubaliano yao walioafikiana katika kikao chao cha pamoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles