30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kinara wa gofu apania ubingwa mashindano ya ‘Nyali Open’

Na MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM


fujqf-zx

BINGWA wa mchezo wa gofu katika michuano ya wazi ya ‘Rwanda Open’, Victor Mbunda, amepania kunyakua ubingwa wa mashindano ya ‘Nyali Open’ yatakayofanyika Desemba mwaka huu jijini Mombasa, Kenya.

Kinara huyo aliyeiwakilisha vyema Tanzania kwenye mashindano hayo yaliyomalizika Jumamosi iliyopita nchini Rwanda, amesema tayari ameanza kuifungia kazi michuano ya Nyali Open.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Victor alisema amepanga kuanza rasmi mazoezi leo kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo ambayo itazikutanisha timu mbalimbali.

“Namshukuru Mungu kwa mara ya kwanza nimeweza kuibuka kinara wa mashindano ya Rwanda Open, lakini kesho ‘leo’ nitaanza mazoezi ili kujiwekea mazingira mazuri ya ubingwa kwa mara nyingine,” alisema Mbunda.

Kwa upande wake, meneja wa mchezaji huyo wa kituo cha Gymkhana, jijini Dar es Salaam, Juma Mlela, aliipongeza Kampuni ya New Habari (2006) Ltd kwa kutoa mwaliko kwa Mbunda na kueleza  kuwa wamejipanga kuhakikisha wanaendeleza ubingwa kwenye mashindano mengine yaliyopo mbele yao.

“Hadi sasa sina wasiwasi na wachezaji wangu kwa mashindano yoyote ya ndani, lakini pia nawatoa shaka Watanzania kwa upande wa mashindano ya kimataifa kutokana na ubingwa tuliopata juzi, tutazidi kupambana ili tufikie malengo,” alisema Mlela.

Mbunda ambaye ni mchezaji wa ridhaa, ataungana na mshindi namba mbili wa  mashindano ya Rwanda Open, Amani Said pia kutoka Tanzania ili kudhihirisha ubora wao katika michuano ya Nyali Open.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles