28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

TEWW yaanzisha jukwaa la kuwasilisha mapendekezo, ripoti

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) imefanikiwa kuboresha mazingira ya tafiti kwa kuanzisha jukwaa la kuwasilisha mapendekezo pamoja na ripoti za tafiti hizo.

Kupitia jukwaa hilo takribani ripoti 12 za tafiti zilizofanywa na wanataaluma wa TEWW ziliwasilishwa.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 24,2022 jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dk. Michael Ng’umbi wakati akiwasilisha taarifa ya Taasisi hiyo ya mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Mkurugenzi huyo amesema taasisi imefanikiwa kuboresha mazingira ya tafiti kwa kuanzisha jukwaa la kuwasilisha mapendekezo pamoja na ripoti za tafiti hizo.

“Kupitia jukwaa hilo takribani ripoti 12 za tafiti zilizofanywa na wanataaluma wa TEWW ziliwasilishwa,” amesema Mkurugenzi huyo.

Aidha,amesema katika kipindi cha mwaka wa Fedha 2021/2022, imeanzisha madarasa 406 ya kisomo ambapo yamenufaisha jumla ya wanakisomo 5,777.

Amesema madarasa wanaendelea kutoa elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi na kuboresha miundombinu ya ufundishaji na ujifunzaji katika mikoa 26 ya Tanzania Bara.

Amesema jumla ya wanafunzi 15,130 (wakike 8,550 na wakiume 6,580) wanaendelea kupatiwa mafunzo hayo.

Amesema mafunzo hayo yalifunguliwa katika shule za msingi za umma katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na yamekuwa yakitumika kama vituo vya mafunzo kwa vitendo na utafiti kwa walimu wanafunzi wa TEWW.

Dk. Ng’umbi amesema kuwa TEWW imeanzisha vituo vinane (8) vipya vya mafunzo na mitihani kwa walimu na wasimamizi wa elimu ya watu wazima wanaojifunza kwa njia huria na masafa katika ngazi za astashahada na stashahada, na kufikisha vituo 77 nchi nzima.

Aidha, Mkurugenzi huyo amesema kuwa wamekusanya takwimu za hali ya kisomo kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na inaendelea na uchambuzi wa taarifa na takwimu hizo ikiwa ni hatua ya mwanzo ya utafiti wa hali ya kisomo na elimu kwa umma nchini.

“Katika mwaka 2022/2023 TEWW itaendelea kutekeleza majukumu yake katika eneo hili, ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwatumia wanachuo wake katika kufungua vituo vya kisomo nchi nzima ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo.

“Kwa mwaka 2022/2023, TEWW itaendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Tekonolojia katika kuandaa Juma la Elimu ya Watu Wazima kwa mwaka 2023,”amesema

Vile vile, TEWW itahamasisha, kusajili na kufundisha wanafunzi 3,000 wa mradi wa SEQUIP kwa mwaka 2023,”amesema Dk Ng’umbi

Hata hivyo Taasisi hiyo imewaomba watanzania
kujiunga na programu za elimu ya watu wazima zinazotolewa na TEWW kwa sababu ni taasisi inayotoa elimu kwa nadharia na vitendo kwa kumjengea mwanafunzi uwezo wa kuwa mtu bora, mwenye uwezo wa kujiendeleza na kupambana na changamoto za maisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles