24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kitongoji cha Nkanka kupata shule, barabara

Na Denis Sekonde, Sogwe

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), David Silinde amesema baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuridhia wananchi wapatao 3,000 wanaoishi katika hifadhi ya msitu wa Ileje Renger katika kitongoji cha Nkanka Kijiji cha Itumba wilayani Ileje kuendelea kubaki, Serikali itaanza ujenzi wa shule  shikizi ya msingi na barabara.

Sehemu ya wananchi wakiwa na timu ya Mawaziri.

Silinde ameyasema hayo leo Oktoba 25, 2022 katika ziara ya kamati ya Mawaziri wa Kisekta inayoshughulikia migogoro ya Ardhi ilipokuwa inaongea wananchi wa kitongoji cha Nkanka, ambao kitongoji hicho kipo katikati ya hifadhi ya msitu wa Ileje Renger na ambao wameishi hapo kwa zaidi ya miaka 40.

Silinde amesema baada ya mchakato wote kukamikika, ujenzi wa shule ya msingi shikizi utaanza na badae itasajiliwa kuwa shule kamili kwa kuwa ni dhamira ya mheshimiwa Rais  kumaliza changamoto zote za miundombinu kwenye sekta ya elimu.

Silinde amesema ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwa ifikapo 2027 changamoto za miundombinu kwenye elimu nchini ziwe zimemalizika kabisa na analeta fedha nyingi za kumaliza changamoto za miundombinu kwenye elimu.

David Silinde amesema Ofisi ya Rais-TAMISEMI inasimamie miradi nmikubwa ya kutatua changamoto za miundombinu katika elimu hapa nchini, ukiwemo mradi Boost una fedha zaidi ya tirioni 1.1 ambazo kazi yake ni nikuboresha elimu ya msingi kwa kujenga shule mpya na kuboresha zilizopo, mradi wa SEQUIP kwa ajili ya kujenga Sekondari mpya kwenye kata ambazo hazina,  mradi wa lipa kulingana  na matokeo (EP4R) 

Kuhusu Barabara ya Nkanka, Silinde amesema baada kumaliza changamoto TARURA Ileje watakuja kuisajili ili Serikali itoe fedha na iweze kutengenezwa vizuri.

Diwani wa kata ya Itumba Mohamed Mwala amesema wananchi wa kitongoji hicho kupelekewa huduma za kijamii zitarahisha wananchi hao kukua kiuchumi sambamba na wanafunzi kufuata masomo karibu.

Agnes Nyondo mwananchi wa kitongoji cha Nkanka amesema baadhi ya viongozi kuwaambia wahamie nchi jirani ya Malawi wamejikuta wanashindwa kufanya mambo ya maendeleo, kama kujenga ,na kulima kwani wamekuwa wakiishi kwa hofu, hivyo wamemshukuru Rais Samia kwa uhamuzi wake wa kuwataka wabaki katika eneo hilo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles