27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Bodi ya mazao mchanganyiko yaanzisha kilimo cha mkataba cha ngano

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko(CPB) imeanzisha kilimo cha mkataba cha zao la ngano katika Mikoa ya Rukwa, Njombe na Makete ili kupunguza gharama ya Sh bilioni 530 kila mwaka inayotumika kuagiza ngano kutoka nje ya nchi.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 24, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Dk. Anselm Moshi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji na mwelekeo wa bajeti ya Bodi hiyo kwa mwaka wa Fedha 2022/23.

Amesema kilimo hicho kinategemewa kuzalisha tani milioni 1 za ngano katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Pia bodi hiyo ipo katika mkakati wa kuwawezesha wakulima wa zabibu mitambo midogo ya kukamua zabibu ili kuuza mchuzi badala ya zabibu zenyewe.

Amesema kuuza mchuzi badala ya zabibu huongezea thamani zao hilo ambalo limekosa wateja kwa miezi kadhaa sasa.

“Katika mpango mkakati wetu tutaingia kwenye zabibu na njia ambayo tunaifikiria ni kuwawezesha wakulima kuwa na mitambo midogo midogo ili wauze mchuzi badala ya zabibu, sasahivi hatufanyi ila kwenye mpango wetu tutafanya,” amesema Dk. Moshi.

Akieleza utekelezaji wa kazi za bodi hiyo Dk. Moshi amesema wana jukumu jukumu la kuhakikisha soko linapatikana hivyo katika mwaka wa Fedha 202/21 bodi imenunua mazao kwa wakulima tani 26,695 yenye thamani ya Sh bilioni 14.8 na kuuza mazao ghafi yenye thamani ya Sh bilioni 12.8.

Aidha, amesema katika mwaka 2021/22 Bodi imenunua mazao kwa wakulima tani 1978.53 yenye thamani ya Sh bilioni 69.8.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles